Staa aliyepata umaarufu sana kupitia soka ambaye kwa sasa anamiliki klabu yake ya Inter Miami, David Beckham amepania kuwanasa mastaa wanaotikisa ulimwengu wa soka Lionel Messi na Cristiano Ronaldo kutua klabuni kwake.
Staa huyu ambaye amewahi kukipiga pale LA Galaxy, anafanya maandalizi ya timu yake kuingia rasmi kwenye soko la soka kwenye ligi inayofahamika kama Major League Soccer msimu ujao. Kuna taarifa zinazotaja mipango yake ya usajili kuelekea shughuli iliyopo mbele yake!
Beckham ambaye pia amewahi kuwa staa wa Manchester United, Real Madrid amekuwa akiweka wazi matamanio yake ya kuwanasa Christiano Ronaldo aliyepo Juventus na Lionel Messi fundi wa Barcelona licha ya kutambua ugumu uliopo kumuondoa Messi Barcelona au kuwashawishi Juventus kumuachia Ronaldo.
Akiweka wazi mipango ya klabu yake na kuwazungumzia mastaa hawa anasema kuwa kila mtu nhuwa na mipango, orodha ya mambo ambayo anahitaji kuyatimiza. Anasema ukiwaangalia Leo na CR7 wanavyocheza unawezaona kama wanakaribia kumaliza soka lao, lakini yeye haoni hivyo. Licha ya kuwa wanacheza soka katika levo kubwa kabisa ni ngumu kuona wakiziacha klabu zao lakini anasema wataangalia, hauwezi jua nini kinaweza kutokea katika soka.



Povel
Gud news
Gabriel
Hao ndo mabingwa wa dunia