Wakati manchester United wanapambana kumsainisha mkataba mpya golikipa David De Gea, sasa wanapata upinzani mkubwa zaidi kutoka Real Madrid wakati ambao Zinedine Zidane amerejea kibarua chake cha umeneja klabuni hapo. Huenda safari ya De Gea kwenda Real Madrid imewadia!
Inafahamika kuwa Bosi Zidane ni mpenzi mkubwa wa golikipa De Gea na anamtupia jicho la pekee wakati akiwa na malengo makubwa ya kukifuma upya kikosi cha Real Madrid kurejesha heshima yake ambayo inaonekana kuyumba kidogo msimu huu.
Real wanasaka kuwa na kikosi bora zaidi kipindi ambacho ndoto za kuchukua ubingwa kwa mara ya 4 zikiwa zimekufa baada ya kupokea kichapo kutoka kwa Ajax kwenye hatua ya mtoano wa timu 16.

Raisi wa Real Madrid, Florentino Perez anaripotiwa kuwa amemuahidi kumpa pesa za kutosha Zidane katika jitihada za kuweka sawa kikosi, dau la paundi milioni 75 linadaiwa kuwa limewekwa kibindoni kwa ajili ya kumnasa David de Gea ambaye mkataba wake na klabu ya Man United unafika mwisho msimu ujao wa joto.
Hata hivyo kuna ripoti kuwa mabosi wa Manchester United kwa sasa wapo kwenye mazungumzo ya mkataba mpya wa nyota huyu unaotajwa kuwa utampa mshahara wa paundi 350,000 kwa wiki na kumfanya awe golikipa anayelipwa pesa nyingi zaidi. Bila shaka De Gea anaweza kujikuta safari yake imeishia Real Madrid kama watampa dili nono zaidi.


Frank Patrick
Ataijutia hii nafasi maisha. Yake yote