Ahadi ya Ole Gunnar kwa Mashabiki Baada ya 2-1

Baada ya kichapo cha bao 2-1 dhidi ya Wolveshampton meneja wa mda wa Manchester United bwana Ole Gunnar ametoa ahadi kwa mashabiki wa United kuwa watarajie makubwa kwa klabu yao kipindi hiki ambacho klabu inakabiliwa na ratiba ngumu kwenye michuano yote.

Baada ya kichapo cha bao 2-1 dhidi ya Wolveshampton meneja wa mda wa Manchester United bwana Ole Gunnar ametoa ahadi kwa mashabiki wa United

Manchester United wameshindwa kuwika walipomtembelea Wolves kwenye robo fainali ya FA Cup, huku mabao ya Raul Jimenez na Diogo Jota kuwaacha Man U wakiondoka na bao la kufutia machozi ambalowalilipata dakika za majeruhi kupitia Marcus Rashford.

Ole Gunnar anasema gemu hii ni gemu ambayo wameonesha soka bovu zaidi toka yeye alipoingia klabuni hapo na anatarajia kuwa wachezaji na yeye watajitathimini ili kupata matokeo mazuri katika gemu zinazofuata baada ya likizo ya kimataifa.

Jota aliyewachapa Man U bao la pili

Ole Gunnar akitoa ahadi kwa mashabiki, anasema kuwa likizo ya kimataifa itatumika vyema na kuwafanya wachezaji wafanye mazoezi zaidi kujiandaa na kazi kubwa iliyopo mbele yao. Bila shaka, huenda wakafanya maajabu kama walivyomtembelea PSG kwenye gemu zinazofuata.

3 Komentara

    Kocha bora.

    Jibu

    Ni noma

    Jibu

    Duh majanga anajiteteah tu huyo

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.