Timu ya Simba imeibuka na na ushindi wa 2-1 dhidi ya As Vita katika uwanja wa Taifa Dar es Salaama na kufuzu kwa hatua ya robo fainali Ligi ya Mabingwa Afrika.
Mabao ya Simba yalifungwa na Mohammed Hussein dakika 36 wakati bao la ushindi lilifungwa Clatous Chota Chama maarufu kama Triple C dakika ya 89.

Goli pekee la As Vita lilifungwa na Kazidi Kasengu dakika ya 13 baada ya uzembe wa mabeki wa Simba kushindwa kuokoa mpira ulikuwa ukizagaa ndani ya eneo la hatari.
As Vita walianza mchezo kwa kasi kitu kilichopelekea mabeki wa Simba kufanya makosa mara kwa mara mpaka Simba waliporejea kwenye kiwango chao na kutawala soka barabara hadi mwishoni mwa kipindi cha kwanza Simba walionekana kuimarika kiufundi.
Kipindi cha pili Simba walirudi kwa kasi ya ajabu na kupeleka mashambulizi kadhaa lango ni mwa As Vita lakini walinzi na golikipa walikuwa imara. Moja ya mabadilko yaliyofanywa na Simba ambayo yameisaidia ni kumtoa Okwi na kuingia Niyonzima ambaye aliongeza ubunifu na kuboresha mashambulizi ya Simba.

Simba sasa wamefuzu robo fainali wakisubiri droo kujua watacheza na nani.
Timu zilizofuzu robo fainali.
Esperance De Tunis Tunisia
Simba Sc Tanzania
TP Mazembe Congo DR
CS Constantine Algeria
Wydadi Casabranca Moroco
Mamelodi Sundowns South Africa
Horoya Guinea
Al Ahly Egypt


Povel
Hongera kwao Simba ya Tanzania