Kiungo mtoto wa Manchester United James Garner amesaini mkataba mpya wa kubakia klabuni Manchester United hadi mwisho wa msimu wa mwaka 2021-22 kukiwa na sharti la maamuzi ya kuongeza mwaka.
Kinda huyu alicheza kwa mara ya kwanza kwenye kikosi kikubwa cha timu hiyo, cha Ole Gunnar Solaskjaer akiwa kama akiba ya dakika za mwisho kwenye gemu dhidi ya Crystal Palace mwezi uliopita.
Staa huyu mwenye miaka 18 pia alikuwepo kama sabu kwenye kikosi dhidi ya PSG wiki iliyopita kwenye gemu ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwenye hatua ya mtoano wa timu 16.

Kinda huyu amekuwepo United tokea akiwana umri wa miaka 8, hivyo ana miaka 10 klabuni hapo. Alikuwa Nahodha wa kikosi cha chini ya miaka 17 cha Uingereza na pia ni mchezaji muhimu kwenye kikosi cha chini ya miaka 18 kwenye gemu inayofuata mwezi ujao kule Dubai.
Ole Gunnar wakati anampa nafasi kinda huyu aliweka wazi kuwa staa huyu anatambua kuwa anaaminika na klabu hivyo atafanya vyema zaidi. Ole Gunnar anamfananisha kinda huyu na kocha Michael Carrick enzi zake.


Povel
Habar njema