Zinedine Zidane amerejea klabuni Real Madrid siku kadhaa zilizopita baada klabu hiyo kuwa na wakati mgumu huu na kufanya maamuzi ya kumtimua aliyekuwa meneja wa klabu hiyo Santiago Solari. Zidane amerejea na anatamani kuwa kocha wa Mbappe!
Siku chache zimepita toka Real Madrid wathibitishe usajili wao wa kwanza klabuni hapoo baada ya kurejea kwa Zidane, ambao walimtaja staa wa FC Porto Eder Militao. Mbappe na Neymar pia wamekuwa wakihusishwa na mabingwa hawa wa Laliga.
Zidane alihojiwa kuhusu taarifa za klabu yake kuhusishwa na mastaa hao wawili na akawa anasita kuzungumzia suala hilo akisisitiza kuwa singependa kuzungumzia wachezaji ambao ni mali ya klabu nyingine. Lakikini pia akasema kiuhalisia angependa kuwa mwalimu wa Kylian Mbappe kama wachezaji wengine mashuhuri.
Real Madrid wanadaiwa kuwa wapo katika maandalizi ya kutumia mkwanja mrefu kwenye usajili unaokuja ili Zidane aweze kusuka upya kikosi chake tayari kwa kurejesha heshima, huenda staa huyu akawa kwenye orodha ya wachezaji wanaopangwa kunaswa na klabu hiyo.



Furahav
Mchukue tu.
isha
Mchukueni tuu sio mbaya
Gabriel
Habar njema sana 👍