Staa wa Liverpool Mohamed Salah amekuwa akiwavutia wapenzi wengi wa soka, ukiacha kiwango alichobarikiwa kinachomfanya awe mmoja wa mastaa bora kabisa wa soka duniani, staa huyu pia amekuwa akiwavutia watu kwa aina ya maisha yake anayoishi. Anatajwa na jarida la TIME kuwa mmoja kati ya watu mashuhuri wenye ushawishi zaidi duniani.

Nyota huyu anaungana na aorodha ya mastaa wengine kutoka tasnia mbalimbali -wasanii wa mziki, wasanii wa filamu, wanasiasa, waandishi na baadhi ya wanaspoti wengine kwenye orodha hii ambayo hutolewa na jarida hili kila mwaka.
Mashabiki wengi sana wamekuwa wakipenda jinsi Salaha anavyoishi bila kujiona kama yeye ni bora sana kuliko wengine na namna anavyoweza kingiliana na mashabiki wake pindi anapopata nafasi ya kufanya hivyo.
Mwandishi John Oliver amemuelezea staa huyu anayetajwa kama “Mfalme wa Misri” kwa ubora wake kuwa amekuwa kama mfano bora kwa watu wa Misri, watu wa Liverpool na waislamu ulimwenguni kwote. Pia amemtaja kama mtu asiyependa majivuno, anayefikiri vyema na mcheshi.
Kwa msisitizo “Salah ni binadamu bora kuliko ubora alio nao kwenye kama mchezaji wa soka” -ameandika mwandishi John Oliver katika makala yake juu ya staa huyu.
Nyota huyu ameungana wanaspoti wengine kama LeBron James, Masters winner Tiger Woods na Alex Morgan kwenye orodha hii, wakiwa kama watu wenye ushawishi duniani.
Salah amekuwa mmoja wa mastaa sita ambao wanapamba ukurasa wa mbele wa jarida la TIME linalowataja watu hawa maarufu na ushawishi wao, amekuwa pamoja na Dwyane Johnson, Taylor Swift, Sandra Oh, Gayle King na Nancy Pelosi



Kenani
Ni kwel kabisa
Fatina mfingi
Hongera yake
Zainabu Kihongosi
Haswaaaa