Hili Liruhusiwe Kwenye Soka?

Kocha wa klabu moja ya Uingereza, katika hali ya kushangaza na kihistoria katika soka, aliwashinikiza wachezaji wake kuwaacha wachezaji wa timu pinzani wafunge goli bila kuwazuia ikiwa kama sehemu ya malipizi ya goli walilowafunga wenzao huku wakishindwa kufuata kanuni ya “fair play”.

Ilikua mechi kati ya Leeds na Aston Villa ambapo Leeds ndiyo walioweza kupata goli mapema huku wakiwa kwao na wakaweza kumuacha mchezaji wa Aston Villa akiwa ameanguka chini huku hajielewi kabisa baada ya kuchezewa vibaya na wachezaji wa Leeds ndani ya mechi hiyo iliyokuwa na ubabe mwingi sana.

Sasa baada ya Leeds United kupata goli hilo la utangulizi ambalo kwa uhalisia halikuwa halali kocha aliwaamuru wachezaji wao kumuacha mchezaji bila ya kumkaba na kuwaacha wapate goli ili kufidiana.

Wenyeji hao wakiwa chini ya Marcelo Bielsa walipata ushindi dakika ya 72 lakini ghafla huku nyota wa Villa, Jonathan Kodjia akiwa chini hana la kufanya. Jambo ambalo liliibua mtafaruku na ugomvi mbele ya muamuzi wa mechi hiyo hadi kupelekea baadhi ya wachezaji kutolewa nje kwa kadi nyekundu.

Baada ya tukio hilo kocha wa Leeds alisikika akiongea kwa sauti akiwataka nyota wale wawaache Aston Villa wafunge goli bila kukabwa akisistiza kwa sauti kubwa!

Baada ya kocha huyo kufanya hivyo nyota wa Villa, Albert Adomah aliweka nyavuni mpira bila kizuizi chochote na kufanya matokeo kuwa 1-1 ndani ya mechi hiyo ambapo ilimfanya hadi Anwar El Ghazi kukutana na kasumba ya kupata kadi nyekundu iliyompeleka nje.

Gumzo ya kilichofanyika bado linabaki pale pale, je, hili suala hili lipo kiufundi katika soka na je, liruhusiwe kupokea maelezo ya aina hiyo endapo kuna ukosefu wa kufuata baadhi ya kanuni za kisoka ambazo kwa hakika ni kipimo cha utu baina ya wachezaji? Na, je, maamuzi ya kocha yalikuwa sahihi kushinikiza wachezaji wake wawaachie wenzao wapate goli rahisi vile bila ulinzi?

Mara kadhaa matukio ya namna hiyo hutokea uwanjani na wachezaji hushangilia kabisa ushindi wanaokuwa nao bila kujua kama kuna mtu amechezewa vibaya ndani ya mechi husika. Hakika wengi tutasifu kocha kwa maamuzi ya kuona kwamba hata kwa hali ya kawaida mechi ingeisha kwa sare na kuamuru kuwaachia wafunge. Huo ndio utu katika soka.

2 Komentara

    Fair play ni muhimu uwanjani

    Jibu

    Huyo ndo kocha bora.

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.