Miamba wa soka wa Congo, TP Mazembe wamesitisha hatua zao za kuendelea kumfukuzia nyota wa Tanzania na klabu ya Young Africa, Ajib ambaye wameona kwamba katika sintofahamu tayari alikuwa amefanya makubaliano na klabu yake ya zamani ya Simba ili mwishoni mwa msimu huu aweze kujiunga nao.
Imeonekana kwamba nyota huyo ameshindwa kukubaliana na baadhi ya vipengele kujiunga na miamba hao mara baada ya kuona pande hizo mbili yaani mchezaji na klabu inayomuhitaji nyota huyo tayari kuna kipengele kipo ndani yake cha makubaliano yake na klabu yake ya zamani.
Katika mazungumzo yaliyofanyika kati ya Andre Mtine wa TP Mazembe na Fredrick Mwakalebela ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa klabu hiyo inaonesha kabisa makubaliano ya usajili wa nyota huyo tayari yamekufa na hakuna uwezekano wowote wa kuyaanzisha upya kwa sasa.
Jambo hilo linatokana na maelezo kwamba Ajib ameamua kurudiana na klabu yake ya Simba na kipengele hicho pekee kimeleta changamoto kubwa sana kwao kuweza kumruhusu kujiunga nao. Pamoja na hilo, bado kuna kila sababu ya nyota huyo kukaa njia moja mbali na vile ambavyo anataka kuchanganya biashara hiyo.
Kocha wa klabu hiyo, Zahera anasema kwamba TP Mazembe wamekuwa wakimtafuta mara kwa mara kutaka kujua kama wangemnasa lakini namna pekee ya kumnasa ni kufuata taratibu zote za kiusajili ndani ya klabu hiyo vizuri na kwa haraka.
Ajib alikuwa ameshaanza kuagana na mashabiki wake kupitia hata mitandao ya kijamii akiwa na imani kwamba safari yake ya kukwea pipa kuelekea Congo imeiva lakini mambo yameenda ndivyo sivyo. Ila hata kusalia kwake hawezi kukosa kabisa nafasi ya kucheza hiyo inatokana na kiwango chake ambacho kila timu inakihitaji.
Alijiunga na klabu ya vijana ya Simba akitokea Boom Fc ya Ilala mwaka 2013 baadaye akaweza kuichezea klabu ya Mwadui katika msimu wa 2014/15 ambapo aliweza kuipa nguvu ya kupanda daraja na kucheza ligi kuu. Hivyo, uwezo wake bado hata Simba wanamhitaji sana kwa matunda zaidi ya klabu yao kwa sababu wanahitaji kukikaza kikosi chao kwa mashindano yajayo.


Tahiya
Haende tyuu hana jipya
Lydia Emmanuel Magoti
Duu Bado ajafika kiwango wanacho kitaka mazembe hapambane watamkubali tuu