Italia watakutana na wenyeji Poland kwenye Kombe la Dunia la vijana U20!
Gemu inapigwa kesho, Jumapili Juni 2, gemu inayoaminika kuwa itakuwa ngumu kwa wageni wakati wenyeji wakipata hamasa kutoka wa mashabiki wa nyumbani.
Italia walifanikiwa kuongoza kundi lao kwa kuwachapa Mexico na Ecuador kisha kutoa sare ya bila kufungana dhidi ya Japan. Wakati huo Poland wamejikuta nafasi ya tatu kwenye kundi lao wakiwa nyuma ya Senegal na Colombia.
Wenyeji wa michuano hii, Poland walichapwa goli 2-0 na Colombia, kabla hawajawachakaza Tahiti kwa bao 5-0. Walitoa sare ya bila kufungana na Senegal kwenye gemu yao ya mwisho na kufuzu kuingia hatua inayofuata.
Msimu uliopita kocha wa U20 Paolo Nicolato aliongoza kikosi chake kupata ushindi wa bao 3-0 dhidi ya Poland Septemba iliyopita. Septemba 2017, pia Italia U20 walishinda bao 6-1 dhidi ya Poland.
Hata hivyo, kocha huyu banaamini kuwa itakuwa ni gemu nzuri na ngumu kwa vijana wake kwa sababu watakuwa wakicheza mbele ya umati mkubwa unaoishangilia timu yao ya nyumbani, bila shaka watajifunza kupitia hilo.
Italia wanaamini Poland ni timu ya tofauti na ile3 waliyokutana nayo vipindi vilivyopita. Wanahitaji kuwa bora zaidi kupata ushindi hapa.
Unataka kutabiri gemu hii? Beti sasa BONYEZA HAPA


Povel
Habar njema