Wakati klabu ya Juventus wakiripotiwa kuwa mbioni kusaini mkataba na meneja wa Chelsea, Maurizio Sarri kuna taarifa kutoka vyanzo tofauti vikiripoti kuwa wakali hawa wanatarajia kuwauza mastaa wawili Joao Cancelo na Mario Mandzukic.

Juve wanatajwa kuwa kwenye mazungumzo na klabu ya Chelsea kusitisha mkataba wa meneja Sarri. Huku wakiwa wanamfukuzia staa wa Tottenham Kieran Trippier.

Kwa mujibu wa Sky Sport Italia na La Gazzetta dello Sport, Sarri hafurahishwi sana na aina ya uchezaji ya Cancelo na angependa staa huyu auzwe kisha wamnunue Trippier anayetajwa kuwa anaendana na aina ya soka la Sarri.

Hata hivyo, staa huyu ambaye Juve wanamtupia macho tayari anatajwa kuwa alikuwa kwenye mazungumzo na Napoli lakini Napoli wakamsajili Giovanni Di Lorenzo kutoka Empoli badala yake.

Dondoo zinataja kuwa mpango wa Juve ni kunasa sahihi kibao kutoka kwa mastaa wa Premier League akiwemo Aaron Ramsey anayetoka Arsenal kama mchezaji huru.

ONI MOJA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa