Montenegro wameamua kumtimua meneja wao Ljubisa Tumbakovic kwa sababu ya kususia kuiongoza timu hiyo kwenye michuano ya kufuzu European Championship. Meneja huyu alikataa kuongoza timu ya taifa hilo dhidi ya Kosovo.
Meneja huyu raia wa Serbia, mwenye miaka 66 anaripotiwa kuwa alipata shinikizo kutoka katika mamlaka za Serbia ambazo haziitambui kosovo kama nchi huru.
Kumekuwa na mvutano kati ya mataifa kadhaa, juu ya husiano za kidiplomasia na kutambua mataifa kutokana na historia zao na changamoto kadhaa za kiuchumi na kidiplomasia. Serbia na Kosovo pia ni ncho ambazo hazijaweka vyema uhusiano wao kidiplomasia, hivyo Serbia hawatambui taifa Kosovo kama nchi huru.
Kosovo inatambuliwa na Marekani na nchi za muungano wa Nchi za Ulaya (EU). Shirikisho la soka la la Montenegro FSCG linamtuhumu Tumbakovic kuwa uamuzi wake wa kutoiongoza timu hiyo ni nje ya maadili ya taaluma yake.
Meneja huyu amekuwa akiiongoza Montenegro tokea mwaka 2016. Uamuzi wake wa kutoshiriki mechi dhdi ya Kosovo uliwahusisha pia wachezaji waweili ambaopia ni raia wa Serbia Filip Stojkovic na Mirko Ivanic ambao pia walisusia kucheza.
Furahav
Anazingua kocha.