Namba 10 ya United Kwenye Historia

Umewahi kuhoji ndani ya viunga vya United juu ya nani aliitendea haki jezi namba 10 uwanjani? Kila shabiki wa United atasema ni jezi yenye historia kubwa sana ndani ya viunga hivyo huku ikiwa imevaliwa na majina makubwa sana kwenye soka. Wengine watakuambia jezi namba 7 ndiyo kila kitu. Waliowahi kuumiliki uzi huo ni:

Dennis Viollet, mwaka 1962 United walivunja rekodi ya usajili baada ya kummiliki nyota wa klabu hiyo kutoka Torino kwa ada ya £115,000. Hii ni kabla mashabiki hawajampa jina la heshima kwa kumbatiza kama King of the Stretford End. Kwa hakika aliifanyia vizuri jezi yake kwenye historia ya klabu hiyo, amemaliza maisha yake ya soka ndani ya klabu hiyo akiwa na magoli 237.

Lou Macari, alijiunga na klabu mwaka 1973 alipotua alikutana na majina hayo ya watu kama Denis ambao ndiyo waliokuwa wababe wa klabu hiyo kwa kipindi chote. Katika msimu wa 1974/75 alikabidhiwa jezi yenye namba hiyo ili kuitumia kila alipopata nafasi ya kuingia uwanjani.

Mark Hughes, miaka ya 1980 nyota huyo alikabidhiwa jezi yenye namba hiyo ikiwa kama heshima kubwa sana ndani ya klabu hiyo. Wengi walihisi nyota huyo angevaa jezi namba 9 lakini hakufanya hivyo na mbadala wake wakampa namba hiyo. Japo hakukaa muda sana mdani ya kikosi hicho na mwaka 1986 alitimkia Barcelona.

David Beckham, wengi husema mchezaji huyo wa zamani wa klabu hiyo anakuzwa sana ndani ya klabu hiyo japo hakuna mafanikio makubwa aliyoyafanya. Jambo hilo siyo sahihi kwa sababu 1995/96 ambapo hapakuwepo na mmiliki yeyote wa namba hiyo alikabidhiwa nyota huyo na kuweza kuitumia vizuri sana ndani ya klabu hiyo. Japo 1997 alipewa jezi namba 7.

Ruud van Nistelrooy, nyota aliyetua kikosini hapo miaka ya 2000 na kuandika historia ya aina yake ndani ya taifa hilo la Uingereza. Katika msimu wake wa kwanza pekee alifunga magoli 36 na wa pili pia akafikisha magoli 44 na kumfanya kujiwekea rekodi ya aina yake. Alitimka klabuni hapo akiwa ameweka kambani magoli zaidi ya 150.

Wayne Rooney, muingereza aliyeweza kuitendea haki jezi yake aliyopewa kwa kipindi kirefu sana. Ni mkongwe kwa klabu hiyo ambaye amejenga heshima ya pekee ndani ya taifa hilo kuanzia kwa mashabiki wa klabu hadi kwa wachezaji wenzake. Aliifungia klabu magoli 245 akiwa nyuma ya mkongwe wa klabu hiyo Bobby Charlton ambaye aliacha historia kubwa na ahadi ya wengi kuivunja.

Makala iliyopita
Makala ijayo

3 Komentara

    Safi sana

    Jibu

    Gud news

    Jibu

    Ipo poa hii

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.