Soka ni mchezo ambao furaha yake ni kuacha alama kubwa ndani ya eneo ambalo makocha ama wachezaji wanakuwa wanapewa kazi kwa kuaminiwa katika nafasi zao. Jambo la pekee kwa kocha ni kutengeneza historia hizo ambazo kwa hakika huwa na lengo la kuisaidia klabu na kuipa maendeleo. Mafanikio ni kitu pekee kinachowatambulisha wachezaji hao ama makocha husika.
Pep Guardiola, sio jambo geni kusikia mkongwe huyo wa kufundisha soka akiwa kwenye nafasi hiyo ya pekee sana. Amekuwa na mafanikio ya wazi kabisa ambayo kwa hakika hayafichiki na yapo wazi. Akiwa ndani ya Barcelona, Bayern Munich na Man City amekuwa na mafanikio ya aina yake ambayo siyo rahisi kuyakataa na kumpa heshima yake kama meneja. Uwezo wake wa kuwatengeneza wachezaji ni mkubwa sana.
Jurgen Klopp, wengi watazungumzia mafanikio makubwa aliyoyapata ndani ya klabu ya Liverpool lakini hiyo siyo historia pekee inayompa heshima kocha huyo. Kwa hakika amejenga historia yake tangu mbali sana hadi kuja kuaminika kama ni kocha mwenye maono chanya ya kisoka. Ameandika historia kubwa ya kunyanyua kombe na klabu ya Liverpool baada ya kuachana na Borussia.
Mauricio Pochettino, kocha anayesifika kwa kutambua viwango na uwezo wa wachezaji wengi ambao kwa nafasi kubwa wasingeweza kuwika katika baadhi ya klabu lakini kwake wameweza kuaminiwa na kupewa nafasi kubwa sana ya kuudhihirishia ulimwengu kwamba wana nafasi kubwa ya kufanya mambo hayo kama wengine. Historia zake zinampa heshima ya aina yake ndani ya klabu hiyo kama msimu uliopita hakufanya usajili lakini akaifikisha pazuri klabu yake.
Diego Simeone, kama ilivyo kwa Jose Mourinho, kocha huyo amekuwa na historia ya aina yake ndani ya Atletico. Ni aina ya makocha wanaowaamini wachezaji kwa kiwango cha aina yake. Anapenda wachezaji ambao kwao utukutu ni kitu cha kawaida sana na katika hilo wanaweza kuleta mafanikio ya aina yake ndani ya klabu kwa kuwa na moyo wa kuipambania klabu zaidi ya mafanikio binafsi.
Jose Mourinho, kocha ambaye amefundisha klabu nyingi sana na kwa mafanikio ya kiwango cha pekee. Klabu nyingi kubwa zinaifahamu historia yake kwa sababu ya aina ya mafanikio ambayo ameacha katika klabu husika. Mara ya mwisho alikuwa kama mwalimu wa United lakini pia klabu nyingine kama Inter Milan, Chelsea na Madrid zote zimeonja mafanikio yake.
Issa
Makocha wa ukweli