Gonzalo Higuain ameanza kufikiria kuhusu uhamisho kuelekea Roma. Kwa mujibu wa chapisho la Corriere dello Sport, nyota huyu hayupo kwenye mpango wa meneja mpya wa Juventus Maurizio Sarri pale Juventus.
Ikumbukwe nyota huyu alikuwa chini ya Maurizio Sarri alipokuwepo Chelsea kwa mkopo. Lakini katika jitihada za kufanya mabadiliko na kuboresha zaidi kikosi cha mabingwa wa Italia, Juventus, Sarri anatajwa kuwa hamfikirii nyota huyu kwenye mpango wake.
Kufutia tumaini dogo la kutokuwepo kwenye kikosi cha Sarri, Higuain anatarajia kuhamia moja ya klabu za Italia, anahusishwa zaidi na klabu AS Roma.
Dili linalotajwa kuweza kufanyika ni kuungana na AS Roma kwa mkopo wa paundi milioni 26 na sharti la kumnunua kwa dau la chini ya paundi milioni 36.

