Siyo wanamichezo wote huwa maarufu kutokana na kile wanachokifanya. Wengine huwa maarufu kwa kipindi fulani tu lakini baada ya kutwaa tuzo husahaulika kwa maana kwamba wanakumbukwa baada ya matukio, kinyume na hapo wanasahaulika kama wapo katika maisha yao kimichezo.
Huwa ni ndoto ya kila mwanamichezo kutengeneza historia ambayo ingemjenga na kumfanya yeye pia aweze kutengeneza kipato kikubwa kupitia umaarufu wake kama ilivyo kwa wanamichezo wengine kama Lewis, Ronaldo, Neymar, Messi ambao umaarufu wao unawapa fungu nono kwa ajili ya kutangaza biashara za wengine. Leo tunakuletea wanamichezo wanaofanya vizuri lakini umaarufu wao ni wa matukio:
Andy Murray
Mchezaji mwenye wasifu mzuri kwenye tenisi akiwa na historia kubwa ya kufanya vizuri sana na ameweka historia nzuri ndani ya Uingereza. Ni miongoni mwa wanamichezo ambao hawatazamwi kwa jicho la pekee. Jambo hili linaanzia hata kwao kutokana na ile hali kwamba endapo atashinda katika mechi au kikombe chochote basi huitwa Muingereza lakini akipoteza ataitwa Mscotland.
Justin Gatlin
Mwanariadha mwenye historia kubwa sana katika michuano mingi mikubwa. Amekuwa na historia kubwa aliyoijenga kwenye riadha lakini pamoja na mataji yake hajaweza kufahamika sana kama ilivyo kwa wenzake akina Bolt ambao wamefanya kitu kilichowajengea jina kubwa mbele ya mashabiki na mbele yao wao wenyewe na taifa lao. Mafanikio aliyoyapata mwaka 2017 mbele ya Bolt hayajampa kabisa ile heshima aliyostahili hadi leo.
Muhammad Ali
Alikuwa ni mwanamasumbwi mkubwa sana aliyeheshimiwa kwa alichokifanya katika kipindi chake chote cha kupanda ulingoni. Mara baada ya kuihama dini yake na kujiunga na Uislamu kulimfanya kusahaulika kabisa kwa kiwango kikubwa. Pia, alichukiwa na wengi baada ya kugoma kushiriki kupambana katika vita dhidi ya Vietnam kukafanya watu kuacha kumfuatilia kwa kiwango kikubwa. Lakini baadaye akaanza kupendwa baada ya kufanya vizuri japo sio sana.
Floyd Mayweather
Ana rekodi ambayo haiwezi kulinganishwa kimafanikio na wapiganaji wengi wa sasa. Ameweza kucheza mapambano makubwa yanayotambulika mengi lakini ameshinda yoye 50-0 mbele ya wapinzani wake aliokutana nao ulingoni. Mbali na utajiri, mali na hata matokeo mazuri aliyonayo hajawa mtu anayeuza sana mitandaoni bila kuwa na tukio linalomfanya ahusike.
Povel tz
Habar njema