Dana Dana Uhamisho wa Neymar

Neymar ametawala vichwa vya habari toka dirisha la uhamisho lilipofunguliwa. Nyota huyu amekuwa akitamani kuondoka klabuni PSG na kurejea klabu yake ya zamani ya Barcelona.

Hata hivyo, suala la uhamisho wa staa huyu limekuwa na dana dana nyingi huku kikwazo kikubwa kikitajwa kuwa ni dau kubwa.

Barcelona walitajwa kufanya mazungumzo na klabu ya PSG, na mpaka sasa wanatarajiwa huenda likatokea jambo kabla ya dirisha la uhamisho kufungwa.

Kwa upande mwingine, Real Madrid nao walikuwa wanaimezea mate sahihi ya staa huyu. Dau la staa huyu linaonekana kutokuwepo kwabisa kwenye mipango ya manunuzi ya klabu hiyo, kama ambavyo waliamua kutemana na Pogba.

Taarifa za hivi punde, kwa mujibu wa L’Equipe zimetaja kuwa Neymar ameamua kuwaambia klabu ya PSG kuwa atasalia klabuni hapo baada ya kushindikana kwa uhamisho kuelekea klabu ya Barcelona.

3 Komentara

    Neymar usiondoke bhuanaa

    Jibu

    Aende tu.

    Jibu

    Gud update

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.