Ndani ya michuano ya klabu bingwa shughuli bado haijafika ukomo wake! Ndiyo kama inaanza kuonekana kupendeza, kutakuwa na vuta n’kuvute ya aina yake ambapo kila klabu itakuwa uwanjani kutafuta tiketi yake ya kuweza kujitetea kuendelea kusalia kunako michuano hiyo, jambo ambalo huzidi kuifanya kuwa bora na yenye mvuto zaidi.
PSG na Real Madrid wanategemewa kumenyana leo katika mechi inayotazamiwa kuwa na ushindani wa aina yake. Wawili hao wana vikosi ghali sana ambavyo kwa aina ya ushindani wao wanaweza kuwa na mechi ambayo kwa hakika itakuwa na kasi ya pekee sana. Madrid bado hawajarudi vizuri kupata muunganiko mkubwa ndani ya kikosi chao jambo ambalo litakuwa na changamoto kwa Zidane, japo hata PSG bado hajwa na kikosi imara kutokana na majeruhi alionao kikosini.
Club Brugge dhidi ya Galatasary, ni mechi ambayo timu zenye majina ya kawaida sana zinakwenda kukutana ambapo ushindani wa timu za aina hii huwa na mechi za pekee sana kutokana na kujuana kwa aina ya wachezaji kila kikosi kinawamiliki kwa wakati husika, japo Galatasary ana nafasi kubwa ya kufanya vyema zaidi katika mechi hiyo.
Olympiacos na Tottenham Spurs, hii huenda ikawa mechi kubwa na ya aina yake kutokana na klabu hizo mbili kuwa katika wakati mzuri kiushindani. Japo Spurs wanapewa nafasi kubwa sana ya kuweza kuibuka na ushindi, lakini linapokuja suala la mechi ya klabu bingwa huwa ni changamoto kubwa sana kutabiri mshindi wa mapema.
Zagreb na Atalanta, hii ni mechi ambayo inawakutanisha klabu ambayo haina uzoefu wa muda mrefu ndani ya michuano hiyo ya klabu bingwa na klabu ambayo huwa na ushiriki japo haijawahi kupata nafasi nzuri sana kuwika katika michuano hiyo. Klabu hizo mbili zitakuwa kibaruani kusaka tiketi ili ziweze kufanya maajabu zaidi kwa kusonga mbele zaidi katika michuano hiyo.
Shakhtar Donetsk uso kwa uso na Guardiola, klabu ya Manchester City imetoka kujeruhiwa katika mechi ya ligi siku za hivi karibuni. Jambo ambalo litafanya mechi ya leo kwao iwe kama sehemu ya kulipa kisasi zaidi ili waweze kufanya vema kwenye michuano hiyo baada ya kulegalega kiasi kwenye ligi.
Mechi nyingine zitakazoshuhudiwa leo ni zile za Atletico Madrid dhidi ya Juventus ambayo inaonekana kuwa mechi kubwa sana kutokana na klabu zinazokutana na aina ya mazingira ambayo zinakwenda kukutana. Leverkusen atakamatana na Moscow ndani ya mechi yao hiyo itakayokuwa na kasi sana dhidi ya wawili hao.


aisha
Ahsante meridianbet
Samiah
Safi sanaa