Baada ya mechi za michuano ya klabu bingwa kwa baadhi ya makundi kuchezwa hapo jana kuna makubwa ambayo yametokea ndani ya hatua hiyo ambapo yapo yaliyoshangaza wengi kutokana na kile kilichotokea na aina ya matokeo yaliyopatikana ndani ya michuano hiyo mikubwa.
Liverpool, ambaye ndiye bingwa mtetezi ndani ya michuano hiyo, alifanywa kitu ambacho siyo rahisi kuamini kwa timu kama yake ile kufungwa idadi ile ya magoli ambayo yalichangiwa na uzembe mkubwa wa safu ya ulinzi baada ya kuwa na mazungumzo mabovu ingawa ana kila linalowezekana kufanya vizuri katika mechi zijazo.
Napoli siyo timu ambayo wanaingia kujaribu uwanjani na hilo linatokana na ukongwe wao na aina ya kikosi ambacho wapo nacho ndani ya msimu huu. Wamekaa kiushindani zaidi ndiyo maana haikuweza kumzuia bingwa huyo wa msimu uliipita kupata upenyo wa kupata hata goli mbele yake. Vijana wa kikosi hicho walionesha umakini wa aina yake uwanjani hapo na kufanikiwa kuibuka na ushindi wa 2-0, ushindi ambao ni mkubwa sana kwa kikosi hicho na kuwaacha Liverpool wakiwa hawana mbinu nyingine kuitumia ili wasawazishe makosa yao kutokana na uimara wa kikosi cha mshindani wake wa msimu uliopita.
Mechi nyingine iliyokuwa na hamshahamsha nyingi ni ile ya Dortmund ambao walikuwa wakiwakaribisha Barcelona. Ndani ya mechi hiyo, Barcelona waliweza kukomaliwa kabisa na Wajerumani hao na kushindwa kuwika kabisa. Mechi ya wawili hao iliweza kuisha 0 – 0.
Chelsea naye alishindwa kabisa kuwika akiwa Darajani baada ya kulazimishwa kufungwa goli na Valencia walioonekana kucheza kwa umoja na mbinu sana mara baada ya kutumia mpira wa faulo ambao ulishindwa kuwafanya mabeki wajue nini cha kwa wakati huo. Matokeo ya mechi yaliweza kuisha kwa 1 – 0.
Matokeo mengine ndani ya mechi za michuano hiyo ni hiyo ni kati ya Ajax; wao waliweza kuibuka na ushindi katika mechi yao, Salzburg aliweza kutembeza kichapo kikubwa na cha aina yake mbele ya Genk ambao walionekana kuelemewa sana ndani ya mechi yao hiyo na kushindwa kufanya maajabu mapema ambayo yanamUweka katika hatua nzuri sana na ya pekee. Benfica nao wakipoteza mechi yao wakiwa nyumbani.


Povel tz
Gud news