Fununu za Soka Barani Ulaya

Klabu ya Manchester United inayoshiriki ligi kuu nchini Uingereza ipo katika harakati za kumfanya mlinda mlango wa klabu hiyo, David de Gea kuwa sehemu ya wachezaji wanaolipwa kiwango cha juu zaidi ndabi ya ligi hiyo ya Uingereza. Mlinda mlango huyo alikuwa akihusishwa na kutimkia katika klabu ya Real Madrid lakini klabu hiyo inataka kutumia ushawishi wa kifedha kuweza kumfanya asalie kikosini hapo kwa miaka mingi zaidi.

Nyota aliyejiunga na klabu ya Real Madrid msimu huu mpya na nyota mwenzake aliyeanza kuitumikia klabu hiyo mapema akitokea Chelsea wanaonesha ushawishi wa aina yake ili kuweza kumfanya kiungo wa klabu ya Chelsea, N’golo Kante kuweza kutimkia katika klabu yao ya Madrid ili aweze kuendeleza majukumu ya kisoka ndani ya klabu hiyo.

Huenda klabu ya Tottenham ikawa katika wakati mgumu kwa kipindi hiki kutokana na nyota wao, Cristian Eriksen kuanza kuonesha kila dalili ya kutaka kuugomea mkataba mpya utakaomfanya aendelee kusalia ndani ya klabu hiyo. Nyota huyo ana kila sababu kutokana na kuhusishwa kwake na kujiunga na klabu kubwa barani Ulaya.

Manchester United wanaonekana kuandamwa na klabu ya Real Madrid mara baada ya kuwepo kwa majaribio kadha wa kadha ya kutaka kumfanya nyota huyo aweze kujiunga na mashetani hao ili iweze kutumika kama mtego wa kumnasa kiungo wa klabu hiyo, Paul Pogba. Nyota huyo kwa namna moja au nyingine amekuwa akivuta umakini wa Madrid na klabu nyingine kubwa barani Ulaya.

Arsenal huenda wakaendelea na kawaida yao ya kusaka vipaji kwa wachezaji wenye umri mdogo mara baada ya kuanza kuhusishwa na kumhitaji kijana anayekipiga ndani ya klabu ya Sunderland, Logan Pye. Nyota huyo amekuwa na kiwango ambacho kinaonekana kushawishi wengi ndani ya ligi kuu ya Uingereza hivyo huenda akaonekana ndani ya klabu hiyo.

Kumeibuka taarifa kwamba huenda klabu za Real Madrid na Barcelona zikachuana sokoni kuwania saini ya meneja wa klabu ya Liverpool, Jurgen Klopp na mlinzi wa klabu hiyo, Van Dijk ili kuweza kujiimarisha zaidi. Wawili hao wanaonekana kuvutiwa na utendaji kazi wa kocha huyo na mlinzi huyo kutokana na uwezo wa watu hao. Endapo wakifanikiwa watakuwa wamevunja rekodi ya pekee sana katika soka.

Makala iliyopita

3 Komentara

    Asante sn kwa taarifa meridianbet

    Jibu

    Hongera sana

    Jibu

    Duuh hatari

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.