KWA sasa mambo yote hadharani juu ya nyota wa klabu ya Barcelona ambaye wengi wanaamini kwamba yeye ni mchezaji wa maisha yote ndani ya klabu hiyo na kwamba hana uwezo wa kuondoka klabuni hapo tena na atastaafu akicheza soka ndani ya klabu hiyo ya Barcelona ambayo amekaa kwa miaka mingi.
Stori imekaa wazi sasa, nyota huyo yupo huru kabisa kwa sasa kuweza kujiunga na klabu yoyote ile anayoitaka wakati wowote ule. Hilo limeonekana wazi katika baadhi ya vipengele vilivyomo katika mkataba wake kwamba yupo huru kabisa kuchagua ni wakati gani angeweza kuondoka klabuni hapo.
Kumbe klabu yake hiyo haikuwahi kuweka pingamizi kwake na kwamba endapo angeamua kuondoka akatafute changamoto nyingine mpya nje ya Barcelona ni jambo ambalo lilikuwa mikononi mwake. Hivyo, hana budi kabisa kuliweka hilo kwenye nia zake kama malengo yake siju moja aihame Barcelona kabla ya kustaafu.
Mshindi huyo wa tuzo ya Ballon d’Or mara tano ambaye ana zaidi ya miaka 19 ndani ya ardhi hiyo ya Hispania yupo huru kuangalia wapi kunamfaa zaidi katika mkataba wake ambao unaisha 2021 japo hazuiliwi kuendelea kusalia ndani ya viunga vya Barcelona ikiwa bado nafsi yake inamtaka kuwa hapo.
Messi alisaini kandarasi na matajiri hao wa jiji la Hispania mwaka 2007 ambayo inamuweka kikosini hapo kwa miaka minne ikiwa na maana kwamba atakuwa huru baada ya hapo huku akiwekewa mtego wenye kuwapa faida Barcelona zaidi endapo kama kuna klabu ingehitaji kuweza kumshawishi ahame.
Baadhi ya mtego uliowekwa ulikuwa ni ada ya kumuondoa kikosini hapo ambayo ilikuwa ni zaidi ya €700m lakini imeonekana kwamba pia kuna uhuru ambao alipewa kuomdoka wakati wowote anaotaka kuondoka katika kikosi hicho kwa kutokumfunga kisoka katika viunga vyao hivyo vya Barcelona, hiyo ina maana kwamba nyota huyo hata kwa msimu ujao yupo huru kufanya maamuzi magumu ya kutimka hapo kama ataamua iwe hivyo.
Hakuna taarifa zozote kutoka kwake kama amefikiria kuondoka klabuni hapo na hata kama atastaafu anaonekana kabisa kufuata nyayo za watangulizi wake akina Xavi na Iniesta kwa kujiunga katika ligi zisizo na ushindani ikiwa ni hatua ya wao kujijenga kimbinu zaidi. Hilo linaweza kuwa chaguo la nyota huyo kwa baadaye zaidi.
aisha
safi sana