Siku ya leo ni ya pekee sana kwa wapenda soka duniani kote kwa sababu mechi kadha wa kadha za klabu bingwa barani Ulaya zitakuwa zikichezwa. Ndani ya mechi hizo kila timu itakuwa ikitafuta nafasi ya kufuzu kucheza michuano hiyo kwa siku za baadaye; jambo ambalo hufanya mechi hizo kuwa na mvuto wa pekee sana. Jicho letu litaangazia kwa marefu mechi hizo.
Napoli dhidi ya Liverpool, wababe hawa siyo mara yao ya kwanza kukutana ndani ya michuano hii. Wanafahamika kwa aina ya soka ambalo wanalicheza pindi wanapokutana uwanjani. Napoli amekuwa mbabe wa Liverpool lakini mara kadhaa imekuwa ni vigumu kwake kupenya na ushindi. Kwa sasa anakutana na Liverpool ambayo ni ya mabingwa wa msimu uliopita.
Salzburg na Genk, Genk siyo wenyeji sana ndani ya michuano hiyo japo ujio wao unaweza kuwa na chachu ya aina yake mara baada ya kuwa na kiwango cha pekee sana kwenye ligi yao kwa msimu uliopita hadi kunyanyua kombe la ligi. Kaa sasa anaingia uwanjani akiwa na wababe hao kutafuta alama zitakazomfanya asonge mbele.
Inter na Slavia Prague, hawa wamekuwa na kiwango cha pekee sana katika kulifanya soka liwe na mvuto ndani ya klabu yao baada ya kufanya usajili ambao unampa nguvu ya kutafuta nafasi ya juu kabisa kwenye michuano hiyo ya klabu bingwa. Uwepo wa watu kama Lukaku na Sanchez ndani kikosi hicho ni chachu kubwa sana ya kutetea ubingwa na kuongeza ushindani pia.
Borussia Dortmund na Barcelona, ni kati ya mechi inayodhaniwa kuwa kubwa na yenye ushindani wa kutosha kutokana na njaa ya kila mmoja kwenye michuano hiyo. Barcelona walifanya vibaya sana katika msimu uliopita na Dortmund ni njaa yake kubwa kutaka kuwa sehemu ya washindani ndani ya kombe la msimu huu.
Mechi nyinginezo zinazotazamiwa kupigwa leo ni Lyon na Zenit ambao watakuwa wakioneshana ubabe, Benfica dhidi ya Leipzig nayo ni kati ya mechi zinazokuwa na ushindani mkubwa sana, Ajax watakuwa wanakipiga na Lille huku mechi nyingine itakuwa kati ya Chelsea watakaokuwa wakimenyana na Valencia katika kusaka nafasi ya kuweza kusonga mbele.
Klabu nyingi zilizo katika nafasi hii ni washiriki wa muda mrefu sana wa kombe hilo hivyo kuna kila linalowezekana ambaye atafanya uzembe wa namna yoyote kuweza kupoteza kabisa nafasi ya yeye kuonesha ushindani wa aina yoyote katika kombe hilo lenye heshima kubwa sana Ulaya na duniani kote.

