Ronaldo Avunja Nyingine!

Kwa mashabiki wa soka wanaposikia tu jina Ronaldo lazima wanaamini kuna kitu kikubwa amekifanya kwa wakati husika. Nyota huyo kwa hivi karibuni amekuwa mtu wa kuweka na kuvunja rekodi nyingi ambazo zilikuwepo kwa kipindi kirefu bila kufikiwa na wachezaji wengi sana.

Ujio wa mchezaji huyo umekuwa wa kipekee sana. Ni mpambanaji na anafanya kila analoweza ili kuhakikisha anakuwa imara na kujiweka kileleni kwa kila analofanya uwanjani. Hadi sasa amefanikiwa kuweka rekodi za kila aina ambazo kizazi kipya cha wanasoka kinatakiwa kuzisawazisha na ikiwezekana kuzipiku kabisa.

Kwa sasa amekuwa akifunga magoli ambayo ni muhimu sana kwa timu zake ikiwa ni ndani ya klabu hata katika timu ya taifa. Umri wake haujawa sababu wala kizuizi cha yeye kuendelea kufanya makubwa zaidi katika soka kwa miaka ya hivi karibuni ukilinganisha na kipindi cha nyuma.

Wengi wanaona nyota huyo ni kama amezaliwa upya maana kadri anavyozidi kusonga mbele kiumri ndivyo anavyoonekana kuwa imara zaidi na anazidi kutisha! Kwa hakika hilo linamuweka yeye tofauti kabisa na wachezaji wengine ambao wakifika umri huo huanza kushuka viwango vyao.

Nyota huyo ameweka rekodi nzito katika mechi ambayo timu yake ya taifa ilikuwa ikicheza na Lithuania kwenye mechi za kutafuta nafasi za kufuzu kucheza michuano ya Euro 2020. Ndani ya mechi hiyo mchezaji huyo alifanya maajabu ya aina yake kwa kufunga magoli manne ambayo yamewapa nafasi nzuri sana Ureno.

Magoli hayo manne ya Ronaldo yanamuweka kwenye nafasi ya juu kabisa ya kuvunja rekodi ya Robbie Keane ambaye ndiye alikuwa akiishikilia rekodi hiyo kwa miaka mingi akiwa ndiye mchezaji aliyefunga magoli mengi katika hatua ya kufuzu kwenye timu yake ya taifa. Anakaa juu sasa akisubiri nyota wengine ambao wanaweza kuvunja rekodi yake kwa siku za hapo mbele akistaafu soka japo siyo jambo linaloweza kuchukua siku chache kutokana na rekodi hiyo ambayo tayari imewekwa. Kwa sasa yeye ndiye kinara wa mabao kwenye hatua hiyo.

Magoli manne ya Ronaldo yamemfanya kufikisha mabao 25 akimuacha Keane ambaye alikuwa na magoli 23. Idadi hiyo Keane aliifikisha akiwa na timu yake ya Ireland. Hadi kuna wakati Keane aliwahi kumuandikia utani nyota huyo kwa kumtaka amuachie rekodi hiyo maana anazo nyingi sana ikiwa kama sehemu ya utani.

3 Komentara

    Nidhamu ya mazoezi ndivyo vimemupa mafanikio#meridianbettz

    Jibu

    Habar njema

    Jibu

    Ronaldo namkubali sana kwanza anajitambua

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.