Mlinda mlango wa klabu ya Manchester United, David de Gea tayari ameweza kutia kandarasi ya kuhudumu ndani ya klabu ya United kwa miaka mitano zaidi na tayari amekwishamwaga wino klabuni hapo ili kuweza kuendelea kuitumikia klabu hiyo ambayo inamhitaji kwa namna yoyote ile.
Barcelona wanaonekana kuanza kuhamisha nguvu upande wa pili, mara baada ya kuonekana kuna ugumu kumnasa Neymar wameanza kuhamishia taarifa na nguvu zao kwa pacha wa mchezaji huyo ndani ya klabu hiyo, Mbappe. Klabu hiyo imeanza kumuwinda nyota huyo ili aweze kuwatumikia kwa misimu ijayo.
Imeweza kufahamika kwamba sababu iliyofanya kocha wa klabu ya Watford aweze kuondoshwa ni kutokana na mengi ambayo yalikuwa yanatokea ndani ya klabu hiyo ikiwemo hata lile la kuwazuia baadhi ya wachezaji kucheza uwanjani na pia, kocha huyo inaonesha aligoma kuimarisha safu yake ya ulinzi ikiwa ni kinyume kabisa na maadili ya kazi yake.
Aliyewahi kuwa kocha wa klabu ya Manchester United, Jose Mourinho ameweza kuzungumzia sakata la Lampard ndani ya klabu ya Chelsea kwa kusema kwamba kocha hiyo anaweza kuwa kati ya viongozi bora kabisa kikosini hapo na akawafikisha pazuri kabisa kutokana na uwezo wake wa kumudu aina ya wachezaji alionao.
Tottenham Hotspurs wanaonekana kutaka kumshawishi kiungo wao, Eriksen kuweza kujiunga na klabu hiyo kwa kumpa kandarasi ambayo inaweza kumlipa donge nono sana la takriban £230,000 kwa wiki kiwango ambacho kwa hakika kina nguvu ya ushawishi. Hiyo ikiwa ni mbinu ya kumzuia kujiunga na klabu za Real Madrid na Manchester United ambazo zinamhitaji.
Valencia na Benfica wapo mbioni kufukuzia saini ya nyota wa klabu ya Crystal Palace, Raymond ambaye amekuwa nguzo kubwa sana ndani ya kikosi hicho. Raia huyo wa Uingereza anawashawishi sana vigogo hao kuweza kumfukuzia kwa nguvu zote.
Mino Raiola ambaye ni wakala wa kuheshimika sana Ulaya anaonekana kutaka kummiliki nyota wa Ivory Coast, Wilfred Zaha ambaye anataka kuachana na mawakala ambao walikuwa wanamsimamia hapo awali. Raiola anamiliki wachezaji wengi wakubwa hivyo haitakuwa kitu kipya kwake kumnasa Zaha.


Povel
Habar njema