Raheem Sterling amekuwa akigonga vichwa vya habari katika wachezaji ambao wanafanya vizuri zaidi. Legendari wa Barcelona, Xavi anafikiri nyota huyu ndiye anayekwenda kuuteka ulimwengu wa soka kama mchezaji maridadi zaidi baada ya Lionel Messi na Cristiano Ronaldo.
Sterling amefanikiwa kuwa na mafanikio makubwa ya soka ya lake akiwa chini ya meneja Pep Guardiola pale Etihad. Ameweza kuvunja rekodi kwa misimu ta 2017-18, na 2018-19 na kuwa moja ya wachezaji muhimu zaidi kwa Manchester City, alifunga jumla ya magoli 35 na kutoa pasi za magoli 21 za magoli katika michezo 67 aliyocheza.
Katika mechi za EPL alizocheza 2019-20, ana magoli matano na amefanya vyema kwenye likizo ya kimataifa ambayo imemuaha na magoli 2 na pasi 4 za magoli.
Xavi anaamini kuwa Sterling atachukua ya Lionel Messi na Cristiano Ronaldo kama mchezaji bora zaidi duniani. Kwa mtazamo wake Xavi, mastaa Ronaldo na Messi watabaki kuwa mfano mkubwa kwenye ulimwengu wa soka.


Lydia Emmanuel Magoti
Safii Sana na mkubali