Etoo Anataka Kushinda UCL Kama Kocha

Samuel Ettoo amesema kuwa anahitaji kushinda Ligi ya Mabingwa Ulaya akiwa kama kocha. Anataka kuwa kocha wa kwanza asiye mweupe kushinda taji hilo.

Ni mwezi huu tuu staa huyu ameamua kustaafu kucheza soka akiwa amefanikiwa kushinda ligi ya mabingwa mara 2 chini ya mameneja Frank Lampard na Guardiola pale Barcelona, na baadaye akweza kushinda taji hilo akiwa klabu ya Inter Milan.

Mshambuliaji huyu mstaafu, ana umri wa miaka 38 na anatamani kumtumia meneja wake wa zamani Pep Guardiola kama mfano wake na kutumia mbinu za kocha huyo kuwinda taji katika ligi ya mabingwa.

Nyota huyu anaamini kuwa ushindi wake utakuwa ni mwanga kwa makocha ambao sio weupe baada ya kukithiri kwa vitendo vinavyoshika kasi vya kibaguzi kwenye soka.

Etoo amesisitiza ujumbe wake dhidi ya ubaguzi wa rangi kwenye soka akisema kuwa licha ya kuwa na rangi tofauti, mwisho wa siku watu wote ni sawa. Etoo anasema kuwa kila mtu kwa nafasi yake anafanya vizuri lakini mara kadhaa kumekuwa na namna tofauti ya kuwatazama watu ambao sio weupe au kupuuzia jitihada na mafanikio yao katika soka.

Ila la kheri Samuel Etoo! Etoo Anataka Kushinda UCL Kama Kocha

Acha ujumbe