Kati ya vitu Chelsea wanasifika kuwa navyo katika kikosi chao ni kumiliki wachezaji ambao wana uwezo mkubwa wa kuhimili mashambulizi ya timu pinzani kwa namna ambayo siyo rahisi kuizuia. Uwezo wa kikosi chao kwenye hatua hiyo wameweza kuwa bora kwa kipindi kirefu na kwa upande wao hilo halipingiki kabisa.
Uwepo wa nyota hao hautufanyi tuamini kwamba wqna safu bora ya ulinzi la hasha bali ni nguvu na uwezo wa nyota mmojammoja katika kutafuta matokeo bora ndani ya kikosi chake. Leo tunakuletea baadhi ya majina ambayo kwa hakika yameweza kufanya vizuri sana ndani ya klabu ya Chelsea kwa kuzuia mashambulizi mengi ya hatari kutokana na ukabaji wao.
Branislav Ivanovic 2008-2017, kwa hakika ni miongoni mwq wachezaji waliojitoa kwa asilimia kubwa sana ndani ya kikosi cha Chelsea. Katika maisha yake ya soka ndani ya ardhi hiyo aliweza kudumu kikosini hapo kwa miaka zaidi ya kumi akiwa kama mchezaji nguli ambaye ameacha historia ndefu ndani ya kikosi hicho.
Ruud Gullit 1995-1998, pamoja na kutua Uingereza akiwa na miaka 32 lakini alikuwa na kitu vha pelee cha kuvhangia ndani ya kikosi kama mchezaji. Kwa hakika juhudi na uwezo wake vilichangia kitu ndani ya kikosi cha Chelsea jambo ambalo liliweza kuwapa nguvu sana upande wa kiungo ambapo ndipo alikuwa anacheza nyota huyo.
Graham Roberts 1988-1990, kati ya watu waliokuwa na ugumu kupitika wakiwa uwanjani nyota huyu alikuwemo pia; na hata alipowahi kuhojiwa juu ya nani anamwogopa zaidi na ni mgumu zaidi kukabana naye aliwahi kusema anajiogopa yeye mwenyewe kutokana na kujiamini kwake ila hajawai kumwogopa mtu mwingine zaidi.
Petr Cech 2004-2015, miongoni mwa walinda mlango wenye umbo linalowapa faida sana wakiwa kwenye majukumu yao ya kuzuia mipira. Pamoja na suala zima la kupata majeraha ya kichwa na kurudi akiwa na helmeti kichwani, hilo halikuweza kumletea matatizo kabisa na alizidi kuonekana nguzo kwa kipindi chote ndani ya kikosi cha Chelsea.
Didier Drogba 2004-2012, 2014-2015, raia huyo wa Ivory Coast kwa hakika ameacha hostoria nzito ndani ya kikosi cha Chelsea. Kwa uwezo wake anakumbukwa kwa alichokifanya wakati wa mechi yao dhidi ya Bayern Munich kwenye fainali ya klabu bingwa alipofunga goli lale na kuipeleka mechi kwenye dakika za ziada; heshima yake ni kubwa mno kikosini hapo.
John Terry 1998-2017, kati ya watu waliojitoa kwa nguvu zao zote ndani ya kikosi cha Chelsea kwenye maisha yao yote ya soka. Alikuwa ni mtu ambaye darajani alipachukulia zaidi ya nyumbani kwa kupambana ili kuhakikisha hawaangushi mashabiki zake kwa kile walichokiamini. Uimara wake ulijenga heshima ndani ya kikosi hicho hakika.


Ester jackson
Chelsea ya zaman ilikuwa ya hatari hakuna ambaye asije jua hili walikuwa na wachezaji ambao walikuwa wanajua wanacho kifanya kwa wakati sahihi sio kama hasaivi