Tunakubali Utani Katika Soka, Ila wa PSG Mnh!

Suala la kuleteana utani, mizaha, kejeli au maneno ya shombo hasa kwa wapinzani katika soka ni jambo la kawaida tu, kwani hutani ndiyo hutoa chachu na hamasa kwa wachezaji kujituma uwanjani na pia mashabiki kujaza viwanja hivyo. Tunaweza sema kama utani katika soka ni kama kachumbari katika pilau au siki kwa mchuzi yaani ina kazi ya kufanya soka lipendeze zaidi. Ila kuna muda huu utani unavuka mipaka na kumfanya anayetaniwa kuhisi amekosewa adabu ijapo akipozwa na kuambiwa ni utani huelewa. Ila utani usizidi, Wazungu wana msemo usemao, “…too much is harmful!” yaani chochote kile kikizidi kina madhara.

Kocha wa Atletico Madrid, Diego Simeone baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya Juventus, aliadhibiwa kwa kushangilia kwa kusimama kisha kuitoa mikono yake kwa nguvu kutoka juu kichwani na kuweka mikono hiyo katikati ya mapaja, huu ni utani ila una maana tata kidogo, akatozwa faini ya paundi 17 000. Mreno, Christiano Ronaldo naye alifanya kama hivyo katika mechi ya marudiano ambao Juventus ilishinda 3-0 na goli zote kufungwa na Mreno huyo, UEFA hawakusita kwani naye walimpa adhabu hiyo hiyo. Uzuri ni kuwa hawa wote wawili wanajuana toka enzi wakiwa mahasimu huko Madrid. Kwa hiyo, mambo yaliisha kimya kimya pasi na shida yeyote.

Tunakubali Utani Katika Soka, Ila wa PSG Mnh!

Mnamo tarehe 18 katika jiji la Dortmund, Haaland aliuwasha moto kweli kweli PSG hawakuamini walichokiona. Kijana mdogo wa miaka 19 kupiga bao mbili mbele ya Neymar Jr , Mbappe na Angel Di Maria ilikua si kazi ndogo. Haaland alipopachika bao la kwanza alishangilia kwa aina yake pendwa ya Yoga, yaani unakaa chini mithili ya mashehe wakiwa wanakula kisha unabana baadhi ya vidole. Kisha akaongeza lile la pili na kufanya matokeo kuisha kwa Dortmund kushinda 2-1 dhidi ya Paris Saint Germain.

Ugomvi ulianzishwa na Dortmund hususan namna ya ushangiliaji wao. Kupitia ukurasa wao wa Instagram waliweka picha ya Haaland kisha waliandika “We don’t buy superstar, we made them!” wakimaanisha kuwa hatununui wachezaji nguli bali wao wanatengeneza hao wachezaji nguli, hii ni kuwapiga vijembe Mbappe na Neymar ambao wamenunuliwa kwa bei kubwa. Kisha naye Haaland akaandika, “Am not in danger; am the dangers” akimaanisha kuwa hayupo kwenye hatari bali yeye ndiyo hatari yenyewe. Vijembe hivi viliwatia hamasa wachezaji wa PSG na kujipa morali ya kujituma zaidi katika mechi ya marudiano ajabu zaidi walikuwa na madukuduku yao moyoni.

Kukaribia mechi ya marudiano Machi 11 kuna ukurasa katika mtandao wa snapchat uliotumia jina la Haaland ulichapisha picha ya Haaland na maneno, “My city, not yours” akimaanisha ni jiji langu, siyo lenu. Maneno yalimkera sana Neymar naye akachapisha kwenye mtandao akisema, “Paris is our city, not yours!” akimaanisha kuwa Paris ni jiji letu sisi, siyo lako. Basi mambo yakawa mambo hatimaye muda wa mtanange ukafika. Ni kweli kebehi, kudharauliwa na kejeli hutia hamasa kwani PSG walifanikiwa kuondoka na ushindi wa bao 2-0. Ajabu ni kwamba Neymar alipofunga bao la uongozi alishangilia kama Haaland, tuseme wazi tu alilenga kumkejeli. Ila mambo hayakuishia hapo kwani hata mpira ulipoisha wachezaji wote wa PSG kasoro Edson Cavani tu walishangilia kwa aina ya Yoga kumdhihaki Haaland.

Haaland

Swali hivi Haaland kawafanya nini mpaka wote wamgeuke na kumuona mbaya? Kama kuchapisha kwenye mitandao hata Dortmund wamechapisha mbona ugomvi wao unamlenga mtu mmoja tu. Ndiyo tuseme wamekerwa na alichochapisha Haaland au wamekerwa na zile goli kumi alizofunga Haaland, maana Neymar na Mbappe wote hawana goli kumzidi dogo huyo.

Baba yake Haaland, bwana Alf Inge alisema, “The are great players but now I will say they lost their humility!” kwamba ni wachezaji wakubwa ila wamekosa utu. Mzee ameonesha ni namna gani wamekosa utu kwa kumshambulia mwanaye kiasi hicho. Kikubwa ni kuwa utani huu umezidi sasa, nahofia kuwa Haaland asijepata sonona au msongo wa mawazo kwa hiki anachokipitia. Hata kama Haaland ndiyo alianza ila ingetosha kwa ushangiliaji wa Neymar ule wa kumdhihaki ila sivyo walivyofanya.

Waswahili husema jambo lisilokuua basi hilo litakupa ukomavu, naamini Haaland atalichukulia hili kama changamoto na atasonga mbele zaidi. Ingekuwa mie Haaland ningeendika, “Ni wivu tu unawasumbua, umeshindwa kuiga mkafunga goli kumi mnaiga aina ya ushangiliaji!” haahaahaa na viemoji au vikatuni vya kuchekacheka huku namalizia na vijembe “Watu wazima hovyo!”

4 Komentara

    Utani nikawaida kwa kipindi kilichopo kwa wakati huo ila wakitoka huwa ndugu kama kawaida

    Jibu

    Ugomvi ulianzishwa na Dortmund hususan namna ya ushangiliaji wao.

    Jibu

    Utani ni kitu kizuri sana.

    Jibu

    Inavutia sana kutaniana

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.