Messi: Nilitaka Kuondoka Barcelona

Nyota wa klabu ya Barcelona, Lionel Messi amekiri kwamba alikuwa hatarini kuondoka ndani ya klabu yake hiyo ya mara baada ya kukutana na masuala mazito ya kodi jambo ambalo liliweza kumfikirisha sana a kufikia hatua ya kitaka kuihama klabu hiyo ili kuachana na masuala hayo ambayo kwake ni mzigo mkubwa.

Taifa la Hispania limekuwa likihusishwa kuwa na kodi ambazo wachezaji wengi wakubwa wamekuwa wakikutana nalo katika hali ambayo inaonekana kuwaumiza sana wachezaji ambao asili yao sio ndani ya taifa hilo. Na limekuwa likifuatiliwa kwa kasi kubwa sana ambapo ni vigumu kwa nyota yoyote kulikwepa.

Nyota huyo wa Argentina na baba yake walikutana na kesi hiyo kwa kusemekana kwamba walikwepa kulipa kodi ndani ya taifa hilo ambayo ilikuwa ikihudiana na haki za picha za matangazo ambapo hutakiwa kulipiwa kwa misingi ya taifa hilo. Baada ya kesi hiyo mchezaji huyo na mzazi wake walikutana na kifungo cha siku 21 ambacho kilikuwa na mbadala wa faini ya kulipa.

Hatua hiyo ya yeye kufikirikiwa na kushtakiwa kwamba aliweza kukwepa kodi kulimfanya atamani kuondoka kabisa klabuni hapo na kulihama kabisa taifa hilo. Lakini changamoto kubwa ilikuja kwake kwamba klabu nyingi zilisita kuweka ofa kwake kwa sababu anafahamika kama mchezaji ambaye moyo wake siku zote upo ndani ya klabu moja, hivyo ingekuwa vigumu sana kumwondoa hapo.

Japo swali bado linasalia wapi ambapo nyota huyo angeweza kutua japo anaweka wazi kwamba, sio kwamba alitaka kuihama Barcelona ila alitaka kulihama taifa la Hispania na hata hivyo hata kama angeweza kuondoka alitaka kujiunga na timu ya ushindi ambayo kwake mataji ni kitu ambacho wanakiangalia sana.

Na kwa uhalisia kauli ya nyota huyo hadi sasa ni kumalizia maisha yake ya soka ndani ya Barcelona na sio sehemu nyingine na anatazamia kustaafu soka lake akiwa na klabu yake ya nyumbani ambayo imemlea na kuweza kumweka katika ramani ya soka Newell’s Old Boys. Huko ndiko anakofikiria kuhitimisha safari yake.

Messi anategemea kuungana na rafiki yake wa muda mrefu Xavi na kwa hakika anatamani endapo siku moja nyota huyo atakuwa kocha ndani ya klabu hiyo kipindi yeye akiwa amestaafu tayari soka. Anaamini nyota huyo atakuwa na mafanikio kama yale ya Guardiola na atakuwa na uwezo kama wao.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.