Ni utamaduni kwa klabu kubwa kuwa na academy ambazo huwa na nia ya kuzalisha wachezaji ambao wataweza kukidhi mahitaji ya kilabu zao au hata kuwauza wachezaji hao nje kwa klabu zenye uhitaji wa wachezaji wa aina hiyo. Miongoni mwa academy zenye majina makubwa duniani ni La Masia ya Barcelona ambayo ilikuwa inamilikiwa na Ajax na baadaye kushikwa na Barcelona na hadi sasa imezalisha zaidi ya wachezaji 400.
Baadhi ya wachezaji waliotoka katika academy hiyo ni Lionel Messi, Gerard Pique, Pedro, Cesc Fabregas ambao wameweza kufanikiwa ndani ya klabu hiyo na wengine wakicheza nje ya klabu hiyo. Pia wengine kama Carles Puyol, Xavi Hernandez, Andres Iniesta, Victor Valdez ambao wengine wanestaafu kucheza soka na wengine wapo nje ya klabu hiyo wakiendeleza uwezo wao wa pekee katika ligi nyinginezo.
Mwaka 2010 waliweka rekodi kwa kutoa wachezaji wao watatu waliokuwa katika hatua za mwisho kabisa za kuchukua tuzo ya Ballon d’Or ambao walikuwa ni Xavi, Messi, na Iniesta. Kwa sasa klabu hiyo inatamani kurudisha baadhi ya nyota wake ili wafanye nao kazi wakiwemo;
Thiago Alcantara (Bayern Munich)
La Masia inasifika kwa kuzalisha viungo wa aina yake ambao kiukweli wanaliteka soka la Ulaya kwa sasa. Uwepo wa wachezaji wenye uwezo kama Thiago unaipa mafanikio makubwa sana Bayern ya sasa ambayo inaangalia namna ya kuweza kurudisha heshima yake ya miaka ya nyuma. Hata akisaini kurudi Barcelona kwake ni kama kurudi nyumbani tu.
Alex Grimaldo (Benfica)
Amekuwa akifananishwa na Jordi Alba kutokana na aina yake ya uchezaji akiwa upande wa kushoto wa uwanja. Ni miongoni mwa nyota waliotabiriwa makubwa ambayo kiuhalisia hadi sasa bado yanaendelea kuonekana kwake kutokana na uwezo wake alio nao. Kwa sasa bado wanajaribu kuangalia kama wanaweza kumfanya tena atue nyumbani kwake hapo.
Andre Onana (Ajax)
Raia huyo wa Cameroon ni miongoni mwa mazao ya klabu hiyo ambaye ameonekana kuwafanya Barcelona kujivunia kutokana na uwezo wake ndani ya uwanja. Mpaka sasa anafanya vizuri na timu yake kwa kuipeleka hatua ya mtoano ya klabu bingwa Ulaya wakionekana kujaribu kufuta rekodi ya ushiriki ya mwaka 1995.
Dani Olmo (Dinamo Zagreb)
Nyota huyo pia anaonekana kuwafanya Madrid waweze kumtamani, hivyo kama Barcelona atajaribu kumrudisha atakutana na upinzani wa matajiri wenzake Real ambao wameuona uwezo wake ndani ya uwanja kwa sasa.


Carolyne
Asante Kwa taarifa
Furahav
Nikwel zinasaidia kupata vipaji vingi.
Neema hassan
Asante kwa makala
Issa
Habari nzuri