Nyota Matajiri wa Nigeria

Nigeria ina wachezaji nyota wengi wanaocheza soka la kulipwa nje ya mipaka ya nchi hiyo. Kwa sababu hiyo wana kipato kikubwa ambacho kinawafanya waweze kutimiza mahitaji yao ya kila siku. Baadhi ya majina ya wachezaji wenye mkwanja mrefu ndani ya taifa hilo ni;

John Mikel Obi

Ana utajiri wa yapata $57M, ni mchezaji ambaye ameweka historia katika soka la kulipwa alianzia maisha yake ya soka katika klabu ya Plateau United na baadae kule Norway, Lyn Oslo. Mwaka 2006 alitaka kujiunga na Manchester United lakini dini hilo liliingiliwa na Chelsea waliotangulia kuinasa saini ya mchezaji huyo. Baada ya kuhudumu kwa miaka 11 ndani ya klabu hiyo aliweza kNigeria ina wachezaji nyota wengi wanaocheza soka la kulipwa nje ya mipaka ya nchi hiyo. Kwa sababu hiyo wana kipato kikubwa ambacho kinawafanya waweze kutimiza mahitaji yao ya kila siku.utimkia China katika klabu ya Tianjin TEDA ambako alitengeneza pesa ya kutosha.

Obafemi Martin

Alianza kucheza soka akiwa na umri wa miaka 19 katika klabu ya FC Ebedei. Ametengeneza utajiri wa $35M ambao ameutengeneza katika klabu mbalimbali Ulaya zikiwemo Inter Milan, Newcastle United na Wolfsburg. Baadaye aliweza kujiunga na ligi ya Marekani ambako nako alikuwa akijikusanyia kitita cha malipo ndani ya klabu hiyo. Vyanzo vikubwa vya utajiri wake ni hoteli anazomiliki katika nchi mbalimbali.

Victor Moses

Ana historia kubwa sana nchini Uingereza ambako amecheza kwa kipindi kirefu sana kwenye maisha yake ya soka. Alianza maisha yake ya soka akiwa na Crystal Palace na baadae kukubalika na klabu ya Wigan Athletic ambako alihudumu hadi miaka ya 2010. Ilipofika miaka ya 2012 aliweza kusajiliwa na Chelsea ambako yupo hadi sasa japo hajawa na kipindi kizuri sana chini ya Sarri. Utajiri wake unakadiriwa kuwa ni $20.1M na amewekeza kwa kiasi kikubwa kwenye ardhi.

Ahmed Musa

Ana historia katika taifa hilo kwa kuwa mchezaji wa kwanza ndani ya taifa hilo kufunga magoli kwenye fainali za kombe la dunia. Musa [26] ameweza kupitia katika klabu mbalimbali katika maisha yake ya soka kwa kuchezea Β GBS Football Academy kabla ya kujiunga na JUTH, Kano Pillars, VVV-Venlo, CSKA Moscow na Leicester City. Utajiri wake unakadiriwa kuwa ni $18M.

Emmanuel Emenik

Alianza maisha yake ya soka kama mshambukiaji lakini ilikuwa ni changamoto sana kwake kufanya vizuri katika nafasi hiyo, lakini hakukata tamaa ya kupambana ili kufanya vizuri katika nafasi hiyo. Amecheza katika soka la Afrika kusini kwa mafanikio makubwa hadi sasa anakumbukwa kwa hilo; kupitia hilo alipata nafasi ya kijikusanyia viwango mbalimbali vya hela ambavyo vimeweza kumfanya atengeneze utajiri wa $18M hadi sasa.

Acha ujumbe