Chelsea Waanza Mazungumzo na Barcelona Kuhusu Countinho

Chelsea tayari imeanza mazungumzo ya siri juu ya usajili wa Philippe Coutinho katika majira ya kiangazi kutoka Barcelona.

Coutinho amehusishwa kurejea Ligi Kuu ya Uingereza majira kiangazi baada ya kushindwa kuonyesha kiwango chake tangu alipotoka Liverpool 2018.

Kiungo huyo wa Brazili anaamini anaweza kubaki Bayern kwa mkopo msimu ujao lakini miamba hiyo ya Bundesliga wameonyesha hawana nia ya kuwa na kipengele cha kumnunua jumla.

Vilabu kama Manchester Unaited, Arsenal na Tottenham pia wamehusishwa kuhitaji huduma ya kiungo huyo, lakini Chelsea tayari wameanza mazungumzo na wawakilishi wa Coutinho.

Barcelona watamuuza kwa dau la £80million, Chelsea wanaamin mahusiano yao mazuri na wakala wake Kia Joorabchian yatafanya dili kukamilika.

Countinho amefunga magoli tisa akiwa Bayern Munich

Boss wa Camp Nou, Quique Setien ameweka wazi kuwa waliwaza Countinho atarejea kwenye klabu na kijiunga na timu ya kwanza.

Lakini kutokana na janga la mlipuko wa Corona, Barca wanahitaji kuuza mchezaji ulikuongeza bajeti ya usajili, mpango ulikuwa kutumia pesa ya mauzo ya Countinho kuwinda mchezaji mwingine sokoni.

2 Komentara

    Habar njema

    Jibu

    Countino hanataka kurudi tena kukicheza uwanja wa EPL dah mashabiki wako tunakusubiri popote utakapo enda na sisi tupo

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.