wa mujibu wa chapisho la Tuttosport, Juventus wanatarajia kuwapiku Liverpool kumpata Ferran Torres kwa kuwapa ofa Valencia ya Mattia De Sciglio au Dabiele Rugani.
Nyota huyu bado ni kinda wa miaka 20, amefikia umri huu wiki chache zilizopit na nafasi yake ni kiungo mshambuliaji. Staa huyu alipenya kwenye kikosi cha kwanza cha Valencia tangia Januari mwaka 2018.
Amechangia kupatikina kwa magoli sita na kutoa asisti saba katika mechi 35 alizocheza za msimu huu na kuwavutia klabu kama Liverpool na wenzie.
Dau la staa huyu kwa sasa linatajwa kuwa Euro milioni 100 kama dau la kumnunua kwa mkataba. Hata hivyo ripoti zinataja kuwa klabu inaweza kupokea Euro milioni 60 kwa sababu Torres amekata kusaini mkataba mpya.
Pia Juventus wanatajwa kuwa wanatarajia kupunguza dau hilo au kuhusisha kubadilishana wachezaji kabisa. Kwa sababu Valencia wanaonekana kuwa na uhitaji wa kuboresha ulinzi kikosini kwao, dili la Juventus kama litahusisha walinzi litakuwa dili bomba zaidi kwao.

