Uwepo wa mchezaji fulani huchochea kwa kiwango kikubwa ari ya mchezaji mwingine kiushindani na hata kimataji. Messi ameweka wazi kwamba siyo siri tena kwake amekumbuka kwa kiwango kikubwa uwepo wa Ronaldo kwenye ligi kutokana na wawili hao kwa pamoja kuweka historia kubwa kwenye ligi hiyo.
Baada ya kuwasaidia Madrid kushinda taji la nne la klabu bingwa Ulaya, nyota huyo aliweza kutimkia zake Serie A kujiunga na miamba wengine wa soka, Juventus. Lakini pamoja na kutimka ndani ya ligi hiyo hakuna kilichopungua kwake kwa sababu anaendekea kufunga kama kawaida na ubora wake bado upo juu kama kawaida.
Lakini upangaji wa pacha unaonesha kabisa kwamba wawili hao hawana nafasi ya kukutana kabisa. Madrid kwa sasa wanajikongoja na Messi ameliona hilo kwa kusema kwamba anakumbuka sana uwepo wa Ronaldo kwa sababu aliifanya La Liga kuwa kitu cha kipekee sana na ilikuwa kwenye mvuto kutokana na ushindani baina yao; japo ilikuwa changamoto kupata mataji kwa urahisi.
Kwake Juventus bado ni klabu sahihi kwa Ronaldo na kutokana na mechi alizozicheza ni dhahiri kwamba hakuna anayeweza kuwachukulia kwa kiwango cha kawaida maana bado wana kikosi kigumu chenye wachezaji wazuri na wenye nidhamu ya kujua nini kinahitajika ili klabu iweze kupata heshima kubwa.
Wawili hao ni miongoni mwa wachezaji ambao wameweka historia kubwa kwenye soka na kila mmoja ameweza kuweka historia ya aina yake. Hili linaonekana wazi na halina kificho kabisa. Japo Messi hajataka kuwasahau wachezaji wengine wa kikosi chake wakiwemo Luis Suarez kwamba nao wana nafasi ya juu wanayochangia kiushindani kwenye ligi hiyo.
Wachezaji wengine ambao Messi anawaona bado wana mchango mkubwa kwake na mbele ya soka ni Neymar, Mbappe, Hazard na Sergio Arguero. Na wanahitaji kupewa nafasi kikosini huko ili kuifanya timu ya taifa lake kuwa imara zaidi.


Furahav
Nikwel ushindani ulikuwa mkubwa sana.
Ester jackson
Kwel kabisa
isha
Kweli ilikua babu kubwa