Kama Messi na Ronaldo Wasingekuwepo

Kuna wakati katika soka wachezaji kadhaa hutokea kuwika sana katika vikosi vyao na kupelekea mashabiki kushindanisha mafanikio yao uwanjani na baadaye huenda mbali sana hata nje ya uwanja pia. Messi na Ronaldo wamekuwa wakishindanishwa kwa kipindi kirefu sana katika historia ya soka vivi karibuni kutokana na mafanikio wanayoyapata na kuyatoa ndani ya klabu wanazopitia wao.

Kuna wakati inatubidi kwenda mbali sana na kuangalia, je, kama hawa wachezaji wawili wangekuwa hawajawahi tokea katika soka nafasi zao zingechukuliwa na akina nani? Jibu la swali hili si kitu ila ni kurejea katika rekodi za wachezaji zilizowahi kuwepo na kufanya makubwa zaidi kipindi cha nyuma.

Hata hivyo, ushindani wa aina hiyo ya wachezaji hauwezi kuvunja uhondo uliopo kati ya hawa wawili maana kwa kiwango kikubwa mafanikio yao yamekuwa makubwa sana kiasi cha kuona kwamba unaweza kujumuisha yale waliyoyapata wachezaji watatu na kuwa mafanikio ya Messi au Ronaldo peke yake.

Katika nafasi ya mfungaji wa muda wote wa klabu bingwa barani Ulaya, ikiwa na maana kinara wa magoli mengi wa muda wote kwa wakati huu nafasi hiyo ingekuwa inashikiliwa na Raúl González mwenye idadi ya magoli 72 akizidiwa na Ronaldo ambaye kwa sasa amefikisha jumla ya magoli 122 ndani ya michuano hiyo.

Katika nafasi ya mfungaji wa michuano ya klabu bingwa Ulaya kwa misimu mingi ya kombe hilo; ikiwa na maana wafungaji ambao wamepata nafasi ya kufunga magoli mengi ndani ya misimu mbalimbali kwenye klabu zao. Nafasi hiyo ingechukuliwa na Van Nistelrooy na Lewandowski qmbao wamefanya vizuri katika misimu mitatu bila kupotea, kwa sasa wanazidiwa na Ronaldo mwenye ubora mkubwa bdani ya misimu sita.

Magoli matatu ndani ya mechi moja [hat-trick] katika michuano ya klabu bingwa barani Ulaya, kama wawili hawa wasingekuwepo kwenye soka basi nafasi yao ingenyakuliwa na Inzaghi, Gomez na Luiz Adriano wenye idadi ya ushindi huo mara tatu; wanazidiwa mbali sana na Messi ambaye amefikisha aina hiyo ya ushindi mara nane kwenye historia yake.

Katika hali ya kawaida tunaweza kusema endapo wawili hawa wangekosekana katika historia ya soka basi kuna uwezekano mkubwa kwamba soka letu tunaloshuhudia sasa katika kipindi hiki lingekuwa tofauti sana tena kwa kiwango kikubwa sana. Kwa sababu tusingekuwa na watu tunaoweza kuwafananisha kwa namba hawa wawili wanafananishwa kwa aina ya mafanikio yao na aina ya ushindani unaofanywa na madhabiki wa soka duniani dhidi yao.

Vitu kama hivi ndivyo huleta radha ya mpira siku zote na huchangia mpira kuwa na hisia za pekee. Baada ya hawa tutegemee kuibuka kwa wawili wengine tena.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.