Aliyewahi kuwa kocha wa Manchester United, Jose Mourinho ambaye aliweza kupumzishwa na uongozi wa timu hiyo kutokana na mwenendo mbovu na matokeo mabovu ndani ya kikosi hicho; bado amekuwa ni mtu wa maneno mengi na anaongea vile anayojisikia na kuanika hali halisi zote anazopitia kwa sasa tangu awe mtu huru.
Kocha huyo anasema tangu atimuliwe na Manchester United hadi sasa alizikataa ofa tatu za kurudi viwanjani kuongoza timu kabla hajajiunga na Spurs. Anajiona ni mwenye furaha na aina hiyo ya maisha kwa sababu yanamfanya ajisikie huru na mwenye uwezo wa kufanya lolote analojisikia yeye. Siyo hivyo tu pia alisema anafurahia maisha yake kwa sababu kurejea kwake uwanjani kunamfanya arudi kwenye mawazo tena kama awali.
Kocha huyo alijaribu kugusia sakata lake la kuondoka ndani ya klabu hiyo ya awali kwamba alikosa ushirikiano wa kutosha kutoka kwa viongozi wake wa juu. Akajaribu kutoa baadhi ya mifano kwamba hata Pep Guardiola wa Manchester City na Juergen Klopp wa Liverpool walipokea ushirikiano wa kutosha kutoka kwa viongozi wao.
Anamzungumzia Klopp kwa kusema alipata msaada wa kutosha klabuni hapo kwa kuruhusiwa kusajili wachezaji wengi sana kama: Alisson Becker, Virgil Van Dijk, Andrew Robertson, Mohamed Salah, Roberto Firmino, Sadio Mane, Fabinho, Georginio Wijnaldum, na Naby Keita kitu kinachowafanya wawe vizuri sana.
Pia, akamzungumzia Guardiola kwamba alipewa ushirikiano wa kuuza na kununua wachezaji anaowataka. Aliweza kuwauza mabeki Zabaleta, Sagna, Kolarov na Clichy huku akisajili wapya kama vile Danilo, Walker, Mendy: kitu ambacho yeye hakuweza kukipata.
Hadi sasa amejiandaa na anazidi kujiandaa kama vile alivyofanya akiwa Inter Milan kwa sababu alifanya makubwa sana msimu ule na hali ile ilimjenga na kujiona ni kocha mwenye thamani kubwa katika soka. Na kwa wakati uliopo anajinoa vizuri ili afanye makubwa kwa timu ya chaguo lake.


Issa
Mournho kocha mzuri sema maneno mengi sana