Kuna baadhi ya wachezaji walio na umri wa chini ya miaka 23 wakafanya mambo makubwa sana katika umri wao. Baadhi ya wachezaji hao wamekuwa nguzo kubwa katika ngazi ya klabu hata timu zao za taifa pia. Tumezoea kuona wachezaji wengi wanafanya vizuri na kuanza kuandika historia zao wanapofikia umri wa jati ya miaka 25 hadi 29 lakini nyota hawa wameanza kukaa kwenye chati za historia mapema zaidi.

Kylian Mbappe

Hadi sasa ana rekodi kubwa kwa kuweza kushinda kombe la dunia akiwa na timu yake ya taifa ya Ufaransa na makombe mengine katika ngazi ya klabu. Hadi sasa katika ligi aliwahi kufunga magoli 17 katika mechi 14 za ligi ya Ufaransa alizozicheza. Kwa aina ya uchezaji wake ana kila sababu ya kufanya vizuri zaidi kwa sasa na hapo mbeleni. Takwimu zake kwa msimu huu zinaridhisha sana kwani amechangia upatikanaji wa magoli zaidi ya 30 ambapo akitoa pasi za magoli zaidi ya 10 na yeye kufumania nyavu zaidi ya mara 21.

Ousmane Dembele

Ni mchezaji wa aina yake anakipiga katika klabu ya Barcelona na umri wake ni miaka chini ya 25 tu ila amekuwa nguzo kubwa ndani ya klabu hiyo. Ni mchezaji mwenye uwezo wa pekee linapokuja suala la kuuchezea mpira kutokana na umaridadi wake wa kutumia miguu yote kwa usawa. Uwezo wa miguu yake miwili umeweza kumfanya afunge zaidi ya magoli 20 kwa mguu wake wa kulia na namba hiyo hiyo kwa mguu wake wa kushoto. Hakika hawa ni tunu ya kutumainiwa ndani ya taifa la Ufaransa.

Jadon Sancho

Alikuwa anakipiga katika klabu ya Dortmund, akawa tishio siyo katika kikisi chao tu bali hata klabu nyingine zilipata shida sana wakati zinapokutana na mchezaji huyu kwa sababu amekuwa akiwapa wakati mgumu hata walinzi akiwa anashambulia. Ni raia wa Uingereza na watu wengi wa taifa lake wanatamani mchezaji huyo angalau angekuwa anacheza ndani ya ligi yao na kuipeperusha zaidi bendera ya taifa lao. Ana umri wa miaka 19. Hizi ni dalili za asubuhi kabisa kwa kikosi cha Uingereza kuimarika zaidi.

Marcus Rashford

Tangu kuondoka kwa Mreno, Mourinho ambaye hakuwa na mapendeleo kumtumia mshambuliaji huyo, nyota yake ilianza kung’aa kwa sasa ndani ya utawala mpya uliopo. Amefanikiwa kufunga magoli matano katika mechi sita alizocheza hivi karibuni; zikiwa ni takwimu nzuri kwa mchezaji huyo raia wa Uingereza.

ONI MOJA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa