UEFA wapo katika mpango wa kuhakikisha wanatengeneza mazingira ya uwezekano wa kumaliza michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya -UCL mwezi Agosti.
Asasi hii kubwa ya michezo Ulaya inatarajiwa kufanya mkutano tarehe 23 April kwa ajili ya kujadili zaidi namna ya kumaliza kampeni ya Ligi ya Mabingwa mwaka huu ambayo imekwamishwa na janga la Corona.
Makubaliano yanayotarajiwa kutoka kwenye mkutano unaokuja ni kumaliza michuano hii mapema iwezekanavyo. Tarehe 29 Agosti ni tarehe inayotupiwa jicho kwa fainali.
Mazingira mazuri yanaangaliwa katika namna ambayo mechi zote zitawezekana kuchezeka mapema na kutoa nafasi katika ligi za nyumbani. Mechi zilizobaki zinaweza kufikiriwa kuchezwa ndani ya wiki mbili.
Changamoto kubwa kwa UEFA ni kwenye upanganyi wa mechi za Ligi ya Europa, ikiwa mechi zote za hatua ya mtoano ya timu 16 zikiwa bado hazijachezwa katika mzunguko wa pili. Mechi zingine mbili zinazohusisha klabu za Hispania na Italia pia bado kwa mzunguko wa kwanza.


Mariam mtandama
Safi