Tottenham yaanza mazungumzo ya wazi na aliyekuwa kocha wao wa zamani Mauricio Pochettino juu ya kupunguzwa kwa malipo ya mshahara wakati huu wa janga la COVID-19.
Pochettino alifungashiwa virago mwezi Disemba mwaka jana na ndani ya masaa 24 baadaye nafasi yake ikabadilishwa na kupewa Jose Mourinho, na kumaliza miaka sita ya utawala wake huko North London.

Inaaminika kuwa mwenyekiti wa Spurs, Daniel Levy ana uhusiano wa karibu na Pochettino na wakati wa kumfukuza kazi Muargentina huyo, alikubali kuendelea kulipa mshahara wake hadi atakapochukua kazi yake inayofuata.
Pochettino bado anaendelea kulipwa mshahara wake wa Pauni milioni 8.5 kwa mwaka, vile vile, Spurs inaendelea kulipa benchi la ufundi la zamani chini ya Pochettino akiwemo Jesus Perez, Miguel D’Agostino na Antoni Jimenez.
Mapema wiki hii Levy alitangaza kubadilisha uamuzi wake wa klabu kutumia Mfumo wa Serikali wa Kulinda Ajira kwa kuwalipa wafanyakazi Asilimia 80 ya mishahara, badala yake klabu itaendelea kuwalipa wafanyakazi wake.
Levy ametoa tahadhari juu ya hasara kubwa za kifedha kwa vilabu kipindi hiki ambapo mechi hazichezwi kutokana na janga la Virusi vya Corona. Spurs pia imeanza mazungumzo na wachezaji wake na kocha Jose Mourinho kuhusu makubaliano ya kupunguza mishahara


aisha
Duuh hatari