Buffon Akubali Dili Jipya Juve

Gianluigi Buffon na raisi wa Juventus Andrea Agnelli wamekubaliana kuongeza mkataba. Kwa mujibu wa Tuttosport, staa huyu amekubali kuongeza mkataba wake Juventus hadi mwaka 2021.

Vetenari huyu mwenye miaka 42 atasalia klabuni hapo baada ya kukamilisha makubaliano kwa njia ya simu na raisi wa Juventus yaliyofanyika wiki iliyopita.

Buffon ameamua kusaini mkataba mpya kwa masharti yale yale ya mkataba wa sasa, hivyo ataongeza mda wake katika soka ili acheze hadi angalau akiwa na miaka 43.

Janga la Corona linakwamisha kumalizika kwa dili hili lakini kwa sasa, lakini repoti inataja kuwa Buffon atasaini mkataba mara moja tu atakapopata nafasi ya kufanya hivyo.

Tuttosport wanasema mchango wa golikipa huyu sio wa kupuuzwa akiwa amecheza jumla ya mechi 11 za michuano yote na kuwa na clean sheet 3.

Golikipa huyu anakuwa mmoja kati ya wachezaji wachache zaidi wenye umri mkubwa waliosalia kwenye soka la kulipwa kwa sasa.

3 Komentara

    Hii iko sawa.

    Jibu

    Habar njema sana 👍

    Jibu

    Asante kwa taarifa meridianbettz

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.