Bundesliga Kurejea Mei 9

Vilabu 36 vya ligi mbili za juu nchini Ujerumani ikiwemo Bundesliga vimesaini makubaliano ya kuendelea na ligi kuanzia Mei 9 mwaka huu kwa masharti maalum ya tahadhari dhid ya virusi vya corona.

Katika baadhi ya viwanja mashabiki wasiozidi 322 wataruhusiwa uwanjani kwa mechi za Bundesliga na mashabiki wasiozidi 270 wataruhusiwa kwa mechi za ligi daraja la kwanza.

Miongoni mwa viwanja ambavyo mashabiki hawataruhuriwa kabisa ni Sgnal Iduna Park kinachotumiwa na Borrusia Dortimund.


Pia wachezaji wote wa timu shiriki wanaokadiriwa kufikia 1,100 watalazimika kufanyiwa vipimo vya Virusi vya Corona kabla ya kuruhusiwa kucheza kila wiki ambapo vitahitajika vipimo zaidi ya 25,000 vitakavyogharimu paundi milioni 2.2 (Tsh. Bilioni 6.3).

Baada ya vilabu kuamua, sasa kinachosubiriwa ni uamuzi wa mwisho kuhusu tarehe hiyo utakaotolewa na serikali baada ya tathmini itakayofanywa na mamlaka za afya nchini Ujerumani.

Kati ya wachezaji 1,100 wenye leseni ya kucheza soka la kulipwa katika ligi hizo mbili nchini Ujerumani, ni wachezaji 14 pekee ambao walibainika kuwa na maambukizi ya virusi vya corona, na wote wameshapona.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.