Spurs imekuwa klabu yenye thamani kwenye Ligi ya Uingereza zaidi kulingana na utafiti mpya uliofanywa hivi karibuni. Unaweza kufikiri Kina Manchester United, Arsenal, Chelsea, Manchester City na wenzake wanapatikana namba ngapi kwenye ripoti hii mpya?
Wakati Klabu ya Spurs ikiwa ni klabu ambayo haipo kwenye orodha ya vilabu vinavyotumia pesa kubwa zaidi kwenye Ligi Kuu ya Uingereza, lakini wameingia kwenye orodha kama vinara kwa klabu zenye thamani zaidi.
Utafiti mpya uliofanywa na Chuo cha Liverpool cha masuala ya utawala chini ya mtaalamu wa masuala ya Fedha Kieran Maguire, unawaweka Spurs mbele ya kina Manchester United, Arsenal, Chelsea, Manchester City ambao wamezoeleka.
Spur wanaongoza na kufuatiwa na klabu ya Manchester City katika nafasi ya pili, wakati nafasi ya tatu ikishikiliwa na klabu ya Manchester United kama vilabu vyenye thamani zaidi.
Licha ya kuwa na uhaba wa mataji, Spurs wameweza kuwapiga gepu wapinzani wao kwenye Ligi Kuu ya Uingereza kutokana na kuwa na matumizi madogo hasa katika mishahara na kumiliki uwanja uliotengenezwa vyema kwa mahitaji ya kibiashara ambayo inawalipa sana.
Katika ripoti yake, Maguire anaelezea kuwa kuna sababu nyingi tofauti zilizowafanya Spurs waweze kupata faida, na ameelezea mazingira ambayo klabu hii imeweza kuwaacha wapinzani wake.
Orodha kamili ya vilabu kulingana na nafasi zao kama ilivyoripotiwa kwenye ripoti mpya.



Ester mmakasa
Nadhani watakua nafasi ambayo watastahili kulingana na mauzo na mapato ya timu zao.
John mwakalosi
Uwanja wao mpya unewaongezea thamani l
Sylvester
Tunatamtaka Kane aje Manchester ili tuwaongezee utajiri zaidi tutakapomnunua
samiah
Inabidi kuonyesha ufundi ktk uwanja mpya
Isaya massawe
Kumbe nao wapowapo