Andress Iniesta na Xavi Hernandez ni zao la Johann Cruyff

Usiku mmoja wa baridi kali April 28, 1988 saa1 usiku, kwenye hotel ya Hesperia, mitaa ya Carrer dels Vergos, Jijini Barcelona nchini Hispania, wachezaji 21 wa klabu hiyo wakiongozwa na kocha Luis Aragones waliweka mgomo kutokana na matendo ya Rais wa Barca, bwana Josep Lluis Nunez.

Ujio wa mwamba wa Uholanzi Johann Cruyff, mnamo Mei 4, 1988 wakiamini kuwa atakuja kufanya mapinduzi makubwa kwenye soka lao.

Siku ya kwanza darasani, Cruyff aliwachorea wachezaji mfumo wa 3-4-3 alioubadili kutoka 4-3-3, wachezaji walishangaa akiwemo Eusebio, dunia hii ya 4-4-2 na 3-5-2 unaleta mfumo mwingine? Waliwaza sana wachezaji wake.

Akili ya Cruyff ilikuwa ni kubadili alichofundishwa na Mwalimu wake Rinus Michels miaka ya 1970 ili kuleta kitu kipya, kumbuka aliuza wachezaji 15 aliowakuta na kuleta wachezaji watakaofit mfumo wake.

Cruyff alimleta winger Txiki Begiristain, Jose Mari Bakero ‘Attacking Midfielder’, Julio Salinas ‘Centre Forward’ na Eusebio ‘Defensive Midfielder’ hawa walikuwa spinal cord ya soka lake, ikumbuke alimbakiza Alexanko ambaye ndie Nahodha na umri wake wa miaka 32.

Wakati anaanza kuisuka Barca mpya kupata ile style ya Barcelonismo aliwahi kumfokea Rais Nunes kutokana na tabia ya kumuingilia kwenye mambo yake, alimwambia ukitaka kuongea na mimi nitakuja ofisini kwako, ila hupaswi kuja dressing room kwangu, mimi ndio Boss hapa

Wakati falsafa mpya inatengenezwa Cruyff aliagiza La Masia yote watumie mfumo wa 3-4-3 kuanzia U8, wakati anaisuka Barca mpya alikuwa na kikosi cha wachezaji vijana, wembamba na wafupi ila yeye ndio aliwahitaji zaidi.

Tuendelee, wakati wachezaji wapo Darasani wakamuuliza, Kocha hapo tunajilinda vipi na mabeki watatu?

ANDRES INIESTA na XAVI HERNANDEZ

Cruyff alijibu kirahisi tu mnataka mabeki wanne wakabe maforwad wawili, mnasahau kuwa tutabaki 6 kwenye kiungo wao wakiwa 8, hapo ni kazi kushinda, “Ukiruhusu kupoteza kiungo umeruhusu kupoteza mchezo”

Wakati Cruyff anasuka trademark akagundua kuwa mfumo wake unahitaji Tactical Artists, mafundi haswa wa mpira, wale football decoraters.

Asubuhi moja pale Camp Nou kulikuwa na wachezaji wanafanyiwa vipimo ambapo mchezaji atakayefikia urefu wa 1.80m atabakishwa, mmoja wapo ambaye hakufikisha alikuwa Pep Guardiola

Kwa Cruyff ilikuwa tofauti sana akaenda La Masia akachukua vijana wembamba, wafupi hata nguvu hawana, watu kama Albert Ferrer, Serge na Guillerme Amor, kuna vitu alivitaka, ile speed, ubora wakiwa na mpira kifupi ni technical giftedness, kumbuka hakuna aliyezidi 1.8m hapo, viongozi walizidi kumshangaa

Cruyff aliweka wazi kuwa hata Pep hakuwa na vigezo vingi vya soka ila vision na ubora wake ndivyo vilimfanya amuamini, he pressed opponents like rats at every angle

Kwa mujibu wa Oriol Domenich ambaye alikaa na timu za vijana za Barca enzi za Cruyff ni kuwa, muda mwingi mazoezi yalikuwa ni kutumia mpira, mpaka pumzi mwamba alikuwa anawatengeneza kupitia mpira.

Kumbuka Cruyff mwenyewe enzi zake alikuwa zaidi ya shetani uwanjani, hivyo wanadai kila mara anasimamisha mazoezi anachora angles na kuwaekeleza wapi walipaswa kukaa wachezaji

Sumu aliyoipika ndio Barca tuliyokuja kuishuhudia ya wakina Andres Iniesta na Xavi Hernandez, zamani Barca hawakuamini kabisa aina hii ya viungo, siku moja alimfuata Pep alimwambia huyu Xavi atakufanya ustaafu mpira, lakini pia alimwaminisha kuwa Andres Iniesta na Xavi watatengeneza pacha moja hatari zaidi duniani kwenye soka.

4 Komentara

    Johann Cruyff was greatest coach

    Jibu

    Kabisaa

    Jibu

    Ni kweli halo Fanya kazi kubwa…..

    Jibu

    Ni kweli halo kafanya kazi kubwa….

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.