Ndemla; Naitazama Simba B ile ya fainali ya BankABC dhidi ya Mtibwa wakiupiga mwingi sana, waliondoka na kombe lao mbele ya Waziri Dk.Fenela Mukangara, kombe akilipokea Nahodha Christopher Edward, pembeni kocha wao Suleiman Matola

Yakutokea yametokea, ni miaka 8 imepita sasa, bado namuwaza kiungo mmoja wa Simba, aliyeuamrisha mpira nini cha kufanya, miguu myepesi sana, akipiga pass fupi na ndefu, akihamisha uwanja atakavyo, alikuwa Michael Ballack kwenye uwanja wa Taifa.
Nafasi ya Ndemla pale msimbazi imekua ni ya kusuasua kutokana na kuepo kwa viungo wa kimataifa kama mwamba wa Rusaka, Tripple C ama kwa jina la gamba au hati yake ya kusafiria anaitwa Cretus Chota Chama ambae akiwa mbele ya Jonas mkude anafanya kibarua chake kua kwenye chungu cha maji ya moto, Changamoto nyingine ni Kiungo mwingine kutoka Sudan bwana Shiboub ambae nae kutokana na Mwili na uwezo wake wa kumiliki mpira bado kunafanya Kocha Sven kuto kuona mchango wa kiungo huyo.
Nyakati zimesogea, muda ukigeuka hata kizuri kinakuwa kinyaa, waswahili walisema, labda ndicho naamini kinachotokea kwa Ndemla na Simba yake, muda umeenda sana hana nafasi ndani ya kikosi ila hajafanya maamuzi


Tahiya
Aendelee tyuu kuwa mvumiliv mana serikal imekubali ombi la kupunguza wachezaji wa kigeni atapata no tyuu
Rehema dickson
Wampe nafasi aoneshe kipaji chake
Ester jackson
Nyakati zimesogea, muda ukigeuka hata kizuri kinakuwa kinyaa, waswahili walisema, labda ndicho naamini kinachotokea kwa Ndemla na Simba yake, muda umeenda sana hana nafasi ndani ya kikosi ila hajafanya maamuzi
Povel
Inabid atafute timu ya kucheza aboreshe kiwango chake kuliko kukaa bench simba
aisha
Majanga hayo tunataka tuuone ujuzi wake msimfanyie hivyo