Klabu ya Ligue 1, Amiens imetuma ombi “kudai haki” baada ya kushuka Daraja kutoka ligi kuu nchini Ufaransa kabla ya msimu kukamilika.
Paris St-Germain walipewa Ubingwa wa ligi siku ya Alhamisi huku Amiens na Toulouse wakishuka daraja baada ya serikali ya Ufaransa kufuta msimu wa michezo wa 2019-20 kwa sababu ya janga la coronavirus.
Amiens walikuwa nafasi ya 19 katika Msimamo wa Ligi, alama nne nyuma ya Nimes na alama 10 mbele ya Toulouse na michezo 10 iliyobaki kucheza.

“Amiens inajiandaa kutuma ombi la kudai haki kwa uamuzi huu muhimu ambao unapingana na mchezo wa haki,” ilisema taarifa.
Ombi hilo litakwenda kwa chombo kinachosimamia ligi, “Ligue de football Professionnel”, kufikiria tena uamuzi wake wa kuwashusha daraja Klabu hizo mbili na badala yake kucheza Ligue 1 na timu 22 badala ya 20 mnamo 2020-21.
Kuwa na timu 22 Kama wanavyotaka ni pamoja na Lorient na Lens, ambao wamepandishwa daraja kutoka Ligue 2..


SADICK
Nasubiri kuona maamuzi ya pingamizi lao. Thanks meridian for information
Gabriel
Madai yao ni kwel kabisa na pendekezo lao n zur maamuz ya busara yanahitajika
hamidu
yap..wanastahili kupata haki yao
povel
jaman wenye zaman ya ligue 1 haki na busara itendeke jaman
David Pere
Kweli watabadisha maamuzi ya awali , Mimi naona hiyo Ndio imeshapita washuke tu
Kenani
Tunasubir mamuz tu
Asia Abdy
Wakubaliane na matokea
mwakalosi
Hili nilijua ya kuwa litatokea sababu kila mmoja anahisi kwa mechi zilizobaki anaweza jitetea
Frank patrick
Kusema kwamba maamuzi yalitolewa bila kushirikisha viongozi wa clubs?…asante meridianbettz kwa taarifa hizi
Rehema Dickson
Wakubali tu kama Wanatakiwa kushuka daraja washuke malumbano ayatakiwi kwenye mpira
Furahav
Wameonewa tu.
felister
haki itendeke
Elika
Hapo ni haki tu na sio vinginevyo
isha
Haki inatakiwa hapo
Issa
Dah pole yao