Leo kwenye kipindi cha SportsRoundUp kinachorushwa na redio ya Clouds Fm kulikuwa na mjadala ambao unaendeshwa na Lwambano pamoja na Amri Kiemba, Luambano aliuliza swali hili Makocha wazawa wanastahili kulaumiwa kwa kushindwa kuwaandaa wachezaji wetu?
“Nilivyoanza mpira wa ushindani, sikucheza sana chini ya walimu wazawa. Kuanzia Kagera Sugar, Yanga, Simba, Azam, hadi Stand United. Baadhi ya walimu wetu hawaamini kile wanachokisomea (kile wanachofundishwa) wanachoamini wao ni namna gani walikuwa wanafanya mazoezi.”

Kwa hiyo mazoezi yao mengi ni kutengeneza mwili lakini sasa hivi mpira umetoka huko umekuja kwenye hesabu na sayance. Hata mazoezi ya siku hizi sio kama zamani kukimbia kama mwanariadha siku hizi mchezaji anatakiwa kukimbia na mpira.
Mazoezi ya siku hizi yanatakiwa kuhususiana moja kwa moja na kitakachotokea kwenye mechi. Kwenye mechi hakuna wakati utakimbia kama upo kwenye riadha, utakimbia na mpira utauachia lakini walimu wengi wa kwetu hawaamini hivyo.
Walimu wetu hawana muda wa kufanyia kazi namna gani timu itacheza. Kwa mfano wiki ambayo mnakwenda kucheza mwalimu atashughulika namna gani wachezaji watakuwa fit kupambana lakini ufundi kama timu hakuna zaidi ya kupanga kikosi na kuwambia tukiwa na mpira tunatanua uwanja tukiwa hatuna tunafinya.
Walimu wa nje wanataka mtu ambaye anaelewa sana, kwa sababu mkishamaliza kujiandaa kwenye Pre-season wakati wa mashindano anafanyia kazi namna gani ya kucheza mechi fulani. Kila mchezo una namna yake kulingana na mechi iliyopo mbele na watu ambao anataka kuwatumia.
Ataangalia nani anaweza kuendana na kitu ambacho, anaweza kuwa amepanga mechi inayokuja atacheza fulani lakini akiona mazoezini huelewi anachoelekeza lazima atabadilisha na kumuka mtu mwingine kwenye hiyo nafasi ambaye anaelewa.
Ndio maana Logalusic alikuwa anawashangaza sana watanzania, anahangaika wiki nzima mazoezi halafu hakioni kile ambacho kakihangaikia wiki nzima mazoezini, anakutoa atakayeingia nae asipofanya kama kocha anavyotaka anatolewa pia.
Makala hii imeandaliwa na Shaffih Dauda


SADICK
Kwa maneno mengine makocha wetu hawaendi na wakati, kwamba mpira umebadilika sana. Asante #meridianbettz kutupatia uhondo
mathayo sonje
kwa upande mwingine tutalaumu sana makocha wa kigeni ama wazawa kwa sababu hata wachezaji wenyewe maandalizi yao sio mazuri maana wajifunza washakomaa kupokea vitu vipya inakua vigumu, nadhani wangeweka program rasmi kutokea vijana wadogo wakakua nao bila kujali wakongwe!!!!
hamidu
ni kweli. makocha wazawa hawajafunzi …hao ndo wanachangia soka letu kubaki nyuma… mpira wa sasa ni uweledi.
Ester mmakasa
Makocha wazawa wanatakiwa nao waende na wakati kwasababu mpira wa umebadilika sio kama zamani ,na pia muda mwingine hata wachezaji wenyewe sio waelewa ,wafwate vile wanavyofundishwa na makocha wao.
Shafii
Makocha wa nyumbani hawaendani na nyakati Sasa kwamba soka linabadilika na sisi inapaswa tuendane na nyakati zilizopo
Elika
Me naona hata hawa wachezaji wetu wanawaelewa zaidi makocha wa kigeni kuliko wazawa,na makocha wa kigeni wanataka wacheza waelewa
Ernest Kimeru
Sasa Ni wakati makocha wetu wa ndani kujifunza mbinu za mpira na kuachana na siasa za mpira.
Frank patrick
Mpira bongo siasa haziwez kuishaa
Povel
Asante meridiana kwa habar za Kimichezo Moto moto
Lombo
makocha wa bongo bado sana maneno meng vitendo ziro lawama nying kwa wachezaj
Emnmy cleopa
Kwa upande mwengine ni kwer makocha wetu hawendani na wakati kwa sababu wengi wao hawana mafunzo mazuri.
Rehema Dickson
Wapewe nafasi wakiwezeshwa wanaweza
aisha
thanks meridianbet for good information
Theckla
Vitu .vingi huwa tunajifunza kutoka kwa wenzetu na hii dhana imeshazoeleka hata kwa wachezaji wetu huwa wanaamini kwamba wakipata mwalimu mgeni bc wataelewa zaidi kuliko mwenyeji
Gabriel
Safi sana