Watakaonunuliwa Endapo Newcastle Ikinunuliwa!

Ikiwa lile sekeseke la klabu ya ligi kuu ya Uingereza, Newcastle United kunuliwa na mabilionea wa Saudi Arabia linakaribia kufikia mwisho,  ni suala la muda tu kabla Newcastle hawajawa kama Chelsea ya Roman Abrahmovich na Manchester City ya Sheikh Mansour.

Bilionea wa Newcastle, Ashley yu mbioni kuachia klabu hiyo kwa mfuko wa Uwekezaji wa Saudi Arabia (PIF) ambao unaongozwa na mwana mfalme Prince Mohamed Bin Salman kwa bei ya paundi milioni 300.

Ikiwa dili hilo litafanikiwa basi tujiandae kuishuhudia Newcastle yenye misuli ya kutosha kushindana katika mbio za ubingwa wa ligi kuu hata kushiriki mashindano makubwa ya Ulaya hasa kutokana na uwekezaji utakaofanywa na bilionea huyo wa Saudia. Kabla hata dili lenyewe halijakamilika kumekua na tetesi za wamiliki hao kutaka kumleta klabuni hapo aliyekua kocha wa Tottenham Mauricio Pochettino. Nyota wa zamani wa Newcastle Mick Martin alinukuliwa na gazeti maarufu la michezo la Uingereza, the Express akimzungumzia kocha huyo, “Pochettino anawajua wachezaji wazuri, anaijua America ya Kusini na Ulaya pia. Ni kocha bora kwa sasa.”

Kama hiyo haitoshi, ili kuimarisha kikosi hicho cha Newcastle United na kukifanya kuwa bora wamiliki hao wameonesha kuhusishwa na wachezaji wafuatao:

Phillipe Coutinho. Watakaokuwa mabosi wapya wa Newcastle wanatajwa kuhusishwa na nyota huyo wa Barcelona anayekipiga kwa mkopo katika timu ya Bayern Munich ya Ujerumani. Kama dili hilo la ununuzi wa timu ya Newcastle United likitimia basi itawalazimu kutoa kitita cha pauni milioni 70 au zaidi ili kupata saini ya nyota huyo.

Nafasi ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 inaonekana kuwa yenye mashaka hivyo anaona ni bora aende sehemu nyingine kutafuta chabgamoto mpya, hakubaliani kuwa mchezaji wa ‘mkopo’. Timu nyingine ambayo itachuana na Newcastle United kwa mchezaji ni Chelsea ya Uingereza.

Antoine Griezmann ni mchezaji mwingine ambaye anatajwa kuwa anaweza kutua St. James’ Park kama mambo yakienda sawa. Jarida la michezo la Sport Mediaset limeripoti kuwa wamiliki wapya wa Newcastle wanavutiwa na nyota huyo wa Barcelona na kuhusu kumnunua ni suala la muda tu kwani pesa kwao sio tatizo.

Moussa Dembele wa Lyon ya Ufaransa ni mchezaji mwingine matata anaetajwa na kuangaliwa sana na mabosi hao. Klabu hiyo ya Newcastle imekua ikihaha kuhitaji huduma ya nyota huyo kila mara na mara zote hizo dili hilo limekua likikwama kutokana na Lyon kuhitaji pesa nyingi ili wamuachie nyota huyo. Kwa ujio wa wamiliki wapya ni wazi kuwa dili hilo linaelekea kutimia kwani wao sio mabahili kama bilionea Ashley ambaye ndiyo mmiliki wa sasa wa The Magpies.

Kylian Mbappe ni mchezaji anaetajwa sana na mashabiki wa Newcastle United lakini sio na viongozi wala wamiliki hao wapya. Mashabiki hao wa The Magpies wanaamini pesa ndiyo kila kitu, kwamba pesa ikiwekwa mezani tu unaweza kufanya kila kitu katika soka. Umtoe Mbappe PSG na kumleta Newcastle, bila shaka wanaamini hata Messi wa Barcelona wataweza kumchukua dili hilo likitimia.

Kwa hili la Mbappe sioni kama kuna uwezekano mkubwa sana wa kutimia kwani kwa umri wa Mbappe ni umri ambao hahitaji kwenda katika timu ambayo ndiyo kwanza inajijenga, anahitaji timu ambayo tayari imeishajijenga ili apate mafanikio katika soka akiwa bado mdogo. Ila wanasema kuwa katika mchezo wa soka lolote linaweza kutokea, tuuachie muda uamue.

John McGinn. Sio tu wachezaji wa nje ya ligi ya EPL tu wanaotajwa, kuna wachezaji kadhaa wa vilabu vya ligi kuu ambao wanatajwa kuhusishwa na Newcastle iwapo dili hilo litakamilika. The Magpies watatakiwa kutoa kiasi cha £20 ili kupata saini ya nyota huyo wa Aston Villa, lakini kikwazo kingine watakachokumbana nacho katika dili hilo ni Manchester United ambao nao wameonesha kuvutiwa na mchezaji huyo.

Dwight McNeil. Moja kati ya timu Zilizotoa ushindani ligi kuu ya Uingereza ni Burnley ambao hawakupewa nafasi kabisa mwanzoni mwa msimu, lakini walichokifanya mpaka sasa sio cha kupotezewa. Burnley  mpaka ligi inasimama walikua nafasi ya kumi katika msimamo wa EPL, mafanikio yao yamechagizwa na uwekezaji uliofanywa na mmiliki wa klabu hiyo tajiri Mike Garlick na juhudi binafsi za wachezaji.

Ukitaja mafanikio ya klabu ya Burnley huwezi kuacha kutaja jina la winga machachari wa timu hiyo Dwight McNeil. Mchezaji huyo ni lulu ya timu hiyo kutokana na kiwango chake kinachokua siku baada ya siku. Kama Newcastle wakifanikiwa kupata saini ya nyota huyu watakua wamefanya usajili mkubwa na muhimu kwa maendeleo ya timu yao.

Tuwaombee mabilionea hao wafanikiwe katika dili lao la kuinunua klabu hiyo ili hizo hela zao za mafuta zipate pa kutumika, mana mara nyingine kuwa na pesa na huna namna ya kuzitumia ni sawa tu na hauna.

51 Komentara

    Asante meridianbet kwa habari zenu

    Jibu

    Itakuwa poa sana

    Jibu

    Kumbe Newcastle inauzwa sikulijua hili asante kwa taarifa meridian

    Jibu

    Now Newcastle watakuwa wacharooo

    Jibu

    Habari za uhakika za michezo tunazipata kwenu meridian bet

    Jibu

    Wachezaji wote ni wazoefu katika soka wanafaa kununuliwa.

    Jibu

    mmetisha sana meridianbet kwa habari mzuri

    Jibu

    Tumuombee afanikiwe kuinunua hiyo klab maana itaongeza ushindano mkubwa kwenye ligi maana ,MBAPE, McNEIL, McGINN, NDEMBELE, na GRIEZMANN Sio poa, hii timu italeta upinzan mkubwa EPL.

    Jibu

    Newcastle watakuwa wameramba dume

    Jibu

    Mnatisha meridian kwa kazi nzuri

    Jibu

    Hii iko poa sana

    Jibu

    Hizi ni taarifa za furaha kabisa kwa Mh.Rais mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete (uncle) na Newcastle yake

    Jibu

    Newcastal itakua Moto wa kuotea mbali

    Jibu

    Hii team itakuwa si ya kitoto ikinunuliwa

    Jibu

    Itakuwa vizuri sana

    Jibu

    Hii safi

    Jibu

    Tuombe wafanikiwe jambo hlo ili epl iwe na ushandi Zaid kwn hv Sasa tuna vita tatu ya kushuka daraja na vita ya ubingwa na top four na Kama watafanikiwah kutakuwah na vita ya top ten ya epl itakuwa tamu Zaid Asante kwa habar ya kimichezo

    Jibu

    tusubili tuone.. kama timu itanunuliwa watakuwa ni timu ya ushindani katika epl & ulimwenguni

    Jibu

    Wapate mtu anaejua kiwekeza kwa kutengeneza team ili ilud kwa ujio wa kasi

    Jibu

    Wainunue waiboreshe ili waweze kuleta uponzani kwenye Epl

    Jibu

    Wamiliki wapya wanaonekana wamejipanga, tutarajie makubwa. Asante#meridianbettz

    Jibu

    Newcastle watakua wameokota embe dodo kwny muarubain

    Jibu

    Itakuwa habari njema kwa mashabiki wa Newcastle

    Jibu

    hii ni habali mbaya kwa skysport na Bt sport

    Jibu

    💰 talks

    Jibu

    Ukiwa na pesa utaitwa majina mengi..hapo pesa tu inaongea

    Jibu

    Ni habari njema Asante meridian

    Jibu

    Itakuwa hatar sana.

    Jibu

    Safi sana, Newcastle itarudisha heshima yake kwenye ulimwengu wa soka!!!!!

    Jibu

    Mnatupatia habari muhimu sana meridian

    Jibu

    Si wakuje Manchester Tu🤸🏻‍♂️

    Jibu

    Hii itakuwa vizur

    Jibu

    Newcastle ipo sokoni duuh

    Jibu

    Itakuwa vizur sana

    Jibu

    itakuwa poa

    Jibu

    Asante meridianbet kwa habari njema

    Jibu

    Mnatutaarifu mambo mazuri asante meridian

    Jibu

    ligi ya england itakuwa na mvuto zaid mana wachezaji watakao chukuliwa n nitishio katika ligi zao

    Jibu

    Mnatuhabarisha sana meridianbet

    Jibu

    Waarabu wana jeuri ya pesa

    Jibu

    Pesa Ipo lakn

    Jibu

    If this deal is approved they will spend so much. Good article @meridianbettz

    Jibu

    Messi kuhama Barcelona watasubiri saana..

    Jibu

    Wachezaji wote wapo sawa

    Jibu

    Good news 👍

    Jibu

    Asante kwa habari nzuri

    Jibu

    Habari nzur safi sana

    Jibu

    Kumbee asante meridianbet kutujuzaa hii habari

    Jibu

    Mambo yatakuwa moto sana

    Jibu

    Wnaonekana Wana pesa sna Hawa jamaa

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.