Danadana Kurejea kwa EPL

Bado kuna dana dana katika maamuzi ya lini haswa Ligi Kuu ya Uingereza itarejea. Mpango na mapendekezo ya wengi ni kurejea mapema Juni, au kabla lakini mpaka sasa mpango huu unaonekana hauwezi kutekelezeka. Klabu za za EPL zinafanya kikao maalumu Jumatatu hii kujadili zaidi.

Mpango wa awali ulikuwa ni kuanza michuano tena bila kuwa na mashabiki uwanjani, na kuhakikisha kila mchezaji, kocha na washirika wote wa uwanja ambao unatumika wanafanyiwa vipimo kwa ajili ya kuhakikisha usalama zaidi wa kila mtu.

Hata hivyo, serikali inatarajiwa kuruhusu mazoezi ya makundi ya wachezaji wachache jumatatu mapema wiki hii. Kwa sasa wachezaji wamelazimika kuendelea mazoezi binafsi. Waziri mkuu arisema kuwa Uingereza wanaruhusiwa kufanya michezo lakini ni kwa washirika wa familia tu.

Kuna mapendekezo ya kutumika kwa “Neutral Venues”, Viwanja vya wote kwa pamoja, sio kila mtu na kiwanja chake. Hata hivyo, mpango huu bado haujakubaliwa na vilabu vyote, na unaonekana kupingwa na karibia timu saba.

Kikao cha leo kinaonekana kupigwa hatua katika mazungumzo na mpango wa kuendeleza ligi. Katibu wa Utamaduni wa Uingereza anatarajiwa kuonana na viongozi wa soka Alhamisi. Hii ni sehemu ya ajenda muhimu.

Danadana Kurejea kwa EPL

Mpaka sasa EPL inaendelea kupata changamoto kadhaa. Mchezaji wa tatu wa Brighton amethibitika kuwa na maambukizi ya Corona, baada ya wawili kuripotiwa kuwa na maambukizi hayo awali.

Mpaka sasa mechi zilizo salia ni 92, na ili mechi zote ziendelee kwa mfumo unaopendekezwa wa kufuata taratibu zote za kitaalamu za kiafya itawagharimu karibu vipimo 40,000, kiasi cha kama paundi 30,000 kwa wiki.

Klabu ya Ulaya kwa ujumla zina hadi tarehe 25 kuwasilisha kwa Uefa kama wanahitaji kumalizia msimu au kusitisha kama walivyofanya League 1. Mkurugenzi mkuu wa EPL Richard Masters alitabiri hasara ya tabribani paundi bilioni 1 ikiwa msimu wa Ligi 2019-20 hautamalizika.

46 Komentara

    Daaa wafanye maamuzi mapema wadau tumemiss kuwaona

    Jibu

    Mashabik tunawasubr kwa hamu kaz ni kwao tu

    Jibu

    tunasubili. burudani ya soka…nategemea waingereza mambo yote yatakuwa sawa

    Jibu

    tumemic haya mambo

    Jibu

    Ila epl vikwazo kibao nao aaaanhh🤨🤨

    Jibu

    Wapenzi wa soka tutafurahi EPL ikirejea. Asante#meridianbettz kutujuza

    Jibu

    Wanasubili nini Sasa waache ianze tu

    Jibu

    Wapenzi wa soka watafurah sana

    Jibu

    Mashabiki tunasubili kwahamu

    Jibu

    Iyo itakua nzuri sanaaa

    Jibu

    Nimess hicho kitu

    Jibu

    Mungu saidia corona iishe kabisa ili tuuendelee kupata raha ya soka letu.

    Jibu

    Habari nzuri

    Jibu

    EPL wana msimamo sana

    Jibu

    ligi hii ipo hatalini kukatishwa maana kwa hizi danadana kunamashaka

    Jibu

    EPL Bora ianze,sababu mashabiki tulisubiri kwa mda mrefu.hata hili janga la dunia litapita na kila kitu kitakuwa sawa

    Jibu

    tunasubiri kwa hamu

    Jibu

    Wafanye maamuzi ili bingwa ananyuyue kwapa #Liverpool

    Jibu

    Bora irud liver achukue kombe lake.

    Jibu

    E.p.L.irudi jamani wadau tumeimis sana

    Jibu

    Safiii hzo danadana ndio tunazozitaka sisi

    Jibu

    Yaani Corona hii sina hamu nayo😭😭

    Jibu

    Wapenz wa soka tutafurahi epl ikianza

    Jibu

    Asante kwa tarifa meridianbet

    Jibu

    Wafanye maamuz haraka tumemic epl kuangaliah

    Jibu

    Iyo itakuwa vizur sana ila Wafanye mahamuzi mapema

    Jibu

    hii hali inawaumiza kichwa sana wafanya maamuzi

    Jibu

    Mko poa sn meridianbet asnte kwa taarifa

    Jibu

    Wafanye maamuz tyuu

    Jibu

    Tunaisubiri na hili janga litapita

    Jibu

    Wanazingua wakati watu tumemisi soka

    Jibu

    EPL ina mambo mengi

    Jibu

    Wafanye maamuz tumic sn epl kuangaliah

    Jibu

    Time for games to start #meridianbettz #meridianbet

    Jibu

    Tunasubiri gem

    Jibu

    Wafanye maamuzi mashabk tumemis kuwaona uwanjan..

    Jibu

    Tunawangoja kwa hamu Sana

    Jibu

    Mungu asaidie mambo yarudi

    Jibu

    Tunasubir

    Jibu

    Wafanye maamuzi mazuri tumewamiss mashabiki wenu

    Jibu

    Tumemiss kuona kandanda warud mapema

    Jibu

    Mapema tu

    Jibu

    Tunawangoja kwa hamuu sana

    Jibu

    Mechi zinakaria kuanza tupate mtonyo #meridianbettz #meridianbet

    Jibu

    Tume miss Aya Mambo jaman

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.