Baada ya kuzaliwa wazazi wake walimpa jina Ronaldo de Assis Moreira. Katika harakati zake za kucheza soka dogo akakuta jina lake Ronaldo ni jina linalotumika na watu wengi basi ikambidi atumie utaratibu uliotumika ili kutofautisha Ronaldo mmoja na Ronaldo mwingine ambao ulikua maarufu pale Brazil kwa kutumia majina ya utani. Utaratibu huo ni kuongeza viambishi fulani katika jina ambavyo vitaendana na mtajwa. Ronaldo mkubwa ataitwa ‘Ronaldao’ na mdogo ‘Ronaldinho’. Lakini pia usisahau kuwa hata hao ‘Ronaldo’ wakubwa kwa wadogo walikua wengi, hivyo yeye akaitwa Ronaldinho Gaucho, yani ‘Ronaldo mdogo kutoka Rio Grande do Sul’.
Hivyo ndivyo kijana Ronaldo akajipatia jina Ronaldinho Gaucho, wavivu na wasio na muda wa kupoteza wakamuita Ronaldinho au Gaucho, Kwao ilikuwa kazi ngumu kuyataja yote mawili kwa wakati mmoja! Unaweza pia ukamuita Dinho, utakuwa sahihi ila punguza uvivu.
Ardhi ya kitongoji cha Porto Alegre kilichopo katika jiji la Rio Grande do Sul ndiyo chimbuko la nyota huyu, bingwa wa matabasamu. Alizaliwa March 21 1980. Kama mtoto wa kawaida anapozaliwa sharti alie basi inawezekana jamaa kwake hali ilikua tofauti na alitabasamu badala yake, Binafsi sijawahi kumuona hana tabasamu usoni. Iwe anapewa tuzo ya mchezaji bora au anaoneshwa kadi nyekundu, amefunga goli au kachezewa rafu yeye anatabasamu tu. Anaweza kukupiga chenga moja ya dharau sana, akakupiga tobo, anatoa pasi halafu anageuka kukuangalia akiwa bado anatabasamu!
Inawezekana fundi huyo hakudumu sana katika viwanja maarufu vya soka, lakini kwa kipindi hicho kifupi alichocheza ameacha alama ambayo haitokaa isahaulike vizazi na vizazi. Alama ya ndui ni ndogo tu lakini haifutiki, ni kama alama aliyoacha Ronaldinho pale PSG na kisha Barcelona.
Samaki ajikunje angali mdogo, Ronaldinho alianza kucheza soka angali kinda wa miaka minane tu! Brazil na soka ni kama Tandale na vigodoro, kuna kiwanja cha mpira kila baada ya nyumba kadhaa. Huko kuna watu wanaucheza mpira, lakini Ronaldo mdogo alionesha kuwa mwiba kati ya hao wote! Moja kati ya tukio ambalo halitowahi kusahaulika ni pale ambapo timu ya mtaani aliyochezea Gaucho ilifanikiwa kuifunga timu pinzani magoli 23-0 huku magoli 23 yote yakifungwa na Ronaldinho peke yake!
Nani angemlaumu kocha wa Gremio kwa kumsajili mchezaji wa kiwango hicho? Naye anajua angemuacha mtaani ingekuwa dhambi ya mpira, dhambi nyingine ni pale alipohitajika na PSG ya Ufaransa yeye angembania..hakuwa tayari kuifanya dhambi hiyo.
Safari ya Ronaldinho haikuishia PSG, iliendelea mpaka Barcelona ambapo aling’ara sana. Akiwa Barcelona Gaucho alifanikiwa kushinda taji la La Liga mfululizo, Ligi ya Mabingwa Ulaya na pia kubeba tuzo ya mchezaji bora wa Dunia ‘Ballon d’Or’. Kisha Ac Milan ya Italia kabla hajarudi nyumbani kwao Brazil kuhitimisha safari ya soka la ushindani na klabu za Flamengo na Atletico Mineiro.
Ukiacha uwezo wake wa kupiga chenga na kasi ya ajabu uwanjani, ufundi wake wa kuwahadaa mabeki na walinda mlango wa timu pinzani pamoja na uwezo wa kuwakera wapinzani kwa mbinu zake za maudhi huku Akiacha furaha machoni kwa watazamaji. Ukiacha historia aliyoiacha ya kuwa miongoni mwa wachezaji wachache wa Barcelona waliowahi kupewa heshima ya ‘Standing ovation’ na mashabiki wa Real Madrid kwenye uwanja wa Santiago Bernabeu katika mechi iliyozikutanisha timu hizo maarufu kama ‘El Classico’ Ronaldinho anakumbukwa na ulimwengu wa soka kwa namna alivyosaidia kumfanya mfalme wa kandanda wa sasa Lionel Messi awe hivi alivyo leo hii.
Ni kweli kwamba Messi ana kipaji kikubwa cha soka, hakuhitaji sana msaada wa mtu mwingine ili awe pale. Lakini hakuna kitu kigumu kama kucheza katika timu kubwa tena iliyojaa wachezaji wenye majina makubwa duniani kama ilivyokuwa Barcelona kipindi hicho huku wewe ukiwa kinda, kitu hicho kilimshinda Neymar. Kucheza chini ya kivuli cha Messi na Suarez. Ronaldinho alimsaidia Messi wa miaka 17 kupita kipindi hicho.
Huyo ndiyo Ronaldinho Gaucho. Muite mchawi wa soka, nabii wa kandanda hata mtume wa mwisho wa mipira. Au jina lolote ambalo litamtofautisha na binadamu yeyote wa kawaida, kwani Gaucho mwenyewevhakuwa wa kawaida.
Akumbukwe Ronaldinho.


Tahiya
Kwer ni mchawi wa soko anajua mno kipindi chake alitisha
Mwanaidi
Yupo vzr sana kwenye soka
felister
Yuko vizuri tangu utotoni magoli 23 peke yake
Povel
Huyu jamaa alikuw mchawi wa soka na dunia kpnd chake thanks meridian kwa information za kisport na burudani
Ernest
Moreira ni kaondoka na ufundi wake.
Dorophina
Alikuwa noma sana kwenye soka uyu jamaa
Mwajuma
Gaucho talent player#meridianbettz
Salma
Yupo vizur i
Lombo
mmmh
Hamidu
Gwiji gaucho anajua sana. Amestaff soka na Mpira wake.# meridianbettz.
winfrida
namkubali sana gaucho yuko vzr
mwakalosi
Mtu ambaye alikuwa ana uwezo wa kuuamrisha mpira ukamtii
Asha
Thnks. Meridian kwa information
Gabriel
Gaucho yuko vzur
SADICK
Gaucho alikuwa fundi uwanjani kwa bahati mbaya alipotea mapema kwa kukosa nidhamu ya kulinda kipaji chake #meridianbettz
Warda
Gaucho mnyama #Meridianbettz
Daniel
crazy story #MeridianBetTZ
Antony Luseno
Gaucho was like a magician when it comes to football
Kenani
Kwel mchaw wa soka
Furahav
Noma sanaaa Gaucho.
Swai
Yuko vizuri sana yan
Emmy cleopa
Gaucho yuko vizur sana #meridianbettz
frank patrick
Fundi kabisa huyu wakibrazil
Shafii
Vitu vya huyo jamaa dimbani vilikua nomaaa
aisha
Gaucho namkubali sana
Lydia Emmanuel Magoti
Gaucho yupo vizuri uyo fundi
Issa
Gaucho aah weka mbali dah