Soka Bila Watazamaji, Chakula Bila Chumvi

Wewe ni golikipa, unafanikiwa kuokoa shambulizi ambalo kiuhalisia lilikua linaelekea kuwa goli. Pengine hata msambuliaji na wachezaji wa timu pinzani kwa ujumla walishaanza kushangilia, au wachezaji wenzako na benchi lenu la ufundi walishaanza kushika vichwa wakijilamu.. Zinasikika kelele kidogo tu zikishangilia na kukupongeza. Unahisi kuna kitu kimepungua, kisha unajikumbusha kuwa ni lile shangwe la mashabiki. Unajua wangekuwepo wangelipuka kwa shangwe na kukupongeza.

Au wewe ni mshambuliaji, unafanikiwa kuwatoka mabeki wa timu pinzani. Unamchukua wa kwanza, wa pili unamdanganya unapita huku kisha unapita kule..yani unatema mate kushoto unafukia kulia. Kisha unabaki wewe na golikipa tu! unaweza kumfunga kwa kumpiga tobo au ukampiga kanzu, unao hata uwezo wa kufunga kwa kisigino. Lakini ukitazama jukwaani unaona viti tupu vikikutizama, hakuna washangiliaji. Unagundua kuwa hakuna haja ya kutia mbwembwe, ni matumizi mabaya ya mbwembwe. Unaamua kubutua tu!, ee nalo si goli tu!

Hakuna tena zile kelele za “usiniumiziee” “ukitoka unione” na nyingine zinazofanana mana hizo! Sasa hivi hakuna tena zile nyimbo za ‘You Will Never Walk Alone’ pale Anfield wala ‘Keep the Blue Flag Flying High’  pale Stamford Bridge!

Chakula bila chumvi, ni sawa na mechi bila watazamaji. “Hakuna kelele (za mashabiki). Unapiga pasi nzuri, unafunga,  lakini hakuna kinachotokea. Ni kero sana” hayo ameyasema Lucien Favre, kocha wa Borussia Dortmund akizungumzia ushindi wa 4-0 wa vijana wake dhidi ya Schlake 04.

Bundesliga imerejea May 16 kwa michezo kadhaa kupigwa. Pamoja na mabadiliko mengi yaliyotokea viwanjani, ikiwa ni katika hatua za kuzuia maambukizi ya virusi vya Corona, lakini mabadiliko makubwa na yenye athari za moja kwa moja katika mpira ni hali ya michezo kuchezwa bila uwepo wa watazamaji. Viwanja vimekuwa vipweke mno!

Kelele zilikua nyingi kudai michezo irudi, watu waliona hata wasiporuhusiwa kwenda viwanjani moja kwa moja kuangalia tu kwenye luninga ingetosha. Haya sasa Bundesliga hiyo imerejea, bila uwepo wa mashabiki watu tumeona namna inavyokua.

Tofauti na siku za kawaida ambapo tulikuwa tukicheki soka huku tukisikiliza na nyimbo za mashabiki, siku hizi ni sauti za wakina Warren Barton, Jim Proudfoot na wengineo wakitangaza na kuchambua mechi hizo zaidi tujiandae kusikia sauti za  makocha na wachezaji wakiongea viwanjani, au sauti ya mpira ukipigwa huku na kule! Shkamoo Corona.

Javier Tebas ambaye ni raisi wa ligi kuu ya Hispania (La Liga) alisema ligi itaendelea June 12, huko Uingereza kuna matarajio ya EPL kurejea June 19, vilabu vya Seria A vimeshapiga kura ligi irejee June 13. Kama hali ya maambukizi ya Corona ikiendelea kuwa hivi tutarajie yale yanayoendelea Ujerumani na Bundesliga yao kutokea hata katika ligi hizo, mechi bila watazamaji.

Belarus wao walishazoea hali hiyo ya kucheza bila watazamaji kwani wao ligi yao haikusimama. Korea Kusini nao wanaelekea kuzoea kwa kuwa nao walisharudi viwanjani tangu wiki kadhaa zilizopita. Shida ipo huku tunakotazama wengi.

Bodi ya ligi pamoja na Bodi ya ligi Bundesliga ‘DFL’ kutoa maelekezo kwa vilabu kuwa wachezaji hawaruhisiwi kushagilia kwa kukumbatiana au kugusana wakati wa mechi, wachezaji wa Hertha Berlin walipomdungua Hoffenheim Kipigo cha mbwa mwizi 3-0 mara kadhaa walijikuta wakisahau marufuku hiyo. Furaha haizuiliki bwana!

Corona imeleta balaa katika soka. Ule msemo maarufu kuwa ‘soka sio mchezo wa gizani’ kidogo unapoteza maana hapa. Na pia hili ni pigo jingine kwa vilabu hasa ambavyo sehemu kubwa ya mapato yake vinategemea viingilio vya watazamaji.

25 Komentara

    Kwer ni sawa na chakula bila chumvi ata hakinogi, tuombe tu mungu ili janga lipite maisha yaendelee

    Jibu

    Ni kwl lakin kpnd hch cha janga la covid 19 (koronA) nivema kwa usalama wa mashabiki na wachezaj Asante meridian bet kwa update

    Jibu

    Ni kwl Ila kwa kpnd hch cha covid 19 (koron) inatubid kuwah na subir kwa usalama wetu na wachezaj ndani ya uwanja thanks meridian bet tz kwa habari za burudani na michezo

    Jibu

    Ni kwl Ila kwa kpnd hch cha covid 19 (koron) inatubid kuwah na subir kwa usalama wetu na wachezaj ndani ya uwanja thanks meridian bet tz kwa habari za burudani na michezo

    Jibu

    true

    Jibu

    Hakuna Radha kabisa..sisi tutashazoea kelele za mashafiki#meridianbettz.

    Jibu

    Tutazoea ni swala la muda kila kitu kitakuwa sawa

    Jibu

    raha ya mpira au michezo ni mashabiki ndo unawapa mzuka wachezaji

    Jibu

    Ni kweli kwa kipindi hiki cha corona yatupasa kuwa wavumilivu..

    Jibu

    Kweli Corona kaharibu mambo

    Jibu

    Yan zile “you’ll never walk alone” na “allez allez “tunazikosaa ila EPL watafanya kitu tu

    Jibu

    Hakika

    Jibu

    Duuuh! Hatar

    Jibu

    Kutokana na hili janga nadhani hapa hakuna ujanja ni hali ambayo wachezaji wanatakiwa kuzoea.

    Jibu

    Hahahahaha bonge la makala #Meridianbettz

    Jibu

    Hahahha haiwezi kunoga hata kidogo

    Jibu

    mpira bila mashabiki hauna radha ata kidogo mashabiki ndo wanapa wachezaji mzuka wa kucheza

    Jibu

    mpira bila mashabiki hauna radha ata kidogo mashabiki ndo wanapa wachezaji mzuka wa kucheza

    Jibu

    Kweli mashabiki wana raha yao wakiwepo uwanjani

    Jibu

    Noma sana.

    Jibu

    Waooo makala safi ahsanteni sana meridianbet

    Jibu

    Ahsante sana meridian kwa taarifa
    #meridianbettz

    Jibu

    Inabidi tuwe wavumilivu katika hili maana hali ya ugonjwa bado ni mbaya ,pindi itakapo kaa sawa mashabiki wataruhusiwa kama ilivozoeleka.

    Jibu

    Ni kweli washangiliaji wanaleta hamasa kwa wachezaji

    Jibu

    Tuwe wavumilivu ugonjwa bado upo Hali bado ijakaa sawa

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.